MKUU wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Jenerali Suleiman Mze(kushoto) leo Julai 18, 2022 amezindua nyumba za makazi ya askari Gereza Ludewa, mkoani Njombe. Nyumba hizo zimejengwa kwa ajili ya kuhudumia familia nne za askari. Aidha, CGP Mzee amechangia pesa kwa ajili ya vigae(Tiles).
MKUU wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Jenerali Suleiman Mze(kushoto) leo Julai 18, 2022 amezindua nyumba za makazi ya askari Gereza Ludewa, mkoani Njombe. Nyumba hizo zimejengwa kwa ajili ya kuhudumia familia nne za askari.
Muonekano wa nyumba za makazi ya askari Gereza Ludewa, mkoani Njombe ambazo zimezinduliwa leo na Mkuu wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee. Nyumba hizo zimejengwa kwa ajili ya kuhudumia familia nne za askari.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee akikagua mashamba ya mahindi katika Gereza la Kilimo Ludewa mkoani Njombe alipotembelea Gereza hilo leo Julai 18, 2022.
Muonekano wa mashamba ya mahindi ya Gereza Ludewa yakiwa katika hatua za kuanza kuvunwa. Gereza hilo ni miongoni mwa magereza 12 ya kimkakati katika uzalishaji wa chakula cha wafungwa kulingana na rekodi yake kiuzalishaji.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee akionja chakula cha wafungwa katika jiko la Gereza Ludewa kama anavyoonekana pichani. Picha zote na Jeshi la Magereza.