Mgeni rasmi wa Bonanza la Maadhimisho ya Siku ya Timu ya Singida Veteran, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Ally Mwendo akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa bonanza hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Mulagiri lililofanyika leo Viwanja vya Peoples mjini hapa leo..
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Ally Mwendo akizungumza na washiriki wa bonanza hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Mulagiri lililofanyika leo Viwanja vya Peoples mjini hapa leo.
Katibu wa Timu ya Veteran Mkoa wa Singida , Gurisha Msemo akizungumza wakati wa uzinduzi wa bonanza hilo lililokwenda sanjari na maadhimisho ya kuanzishwa kwa timu hiyo.
Timu zikiwa uwanjani.
Wachezaji wakiwa uwanjani.
Bonanza likiendelea.
Bonanza likiendelea.
Timu picha ya pamoja.
Timu zikiwa Uwanjani.
Waamuzi wakiwakatika picha ya pamoja.
Mmenyano ukiendelea uwanjani.
Mtifuano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WACHEZAJI wa Timu ya Veteran Mkoa wa Singida wameadhimisha kuanzishwa kwa
timu hiyo kwa kufanya bonanza la mchezo wa miguu na timu za maveteran kutoka
mikoa ya Tabora na Dodoma mchezo uliofanyika Viwanja vya Peoples mjini hapa.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu wa Timu hiyo Gurisha
Msemo alisema maadhimisho hayo yalikwenda sanjari na uhamasishaji wa zoezi la
sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu nchini kote.
” Katika kuadhimisha siku hii moja ya kazi tulioifanya ni kuwatembelea
watoto Yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu wanaolelewa Kituo cha
Upendo Hope kilichopo mjini hapa na
kuwapa zawadi mbalimbali” alisema Msemo.
Mgeni rasmi wa bonanza hilo Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Ally
Mwendo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Paskas Mulagiri
aliwapongeza Veteran Singida kwa kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Mwendo alitaja baadhi ya faida za michezo kuwa ni afya, inajenga urafiki,
undugu na ushirikiano pia ni ajira hivyo kila mtu anapaswa kuicheza.
“Lakini kama tunavyofahamu na kushauriwa na madaktari kuwa
kunamagonjwa yasiyoyakuambukiza ambayo yanatoka kwa kufanya michezohivyo
nawapeni hongera kwa kulijua jambo hilo” alisema Mwendo.
Aidha Mwendo alisema kama tunavyoona jinsi wanavyoshirikiana kati ya
maveteran kutoka Tabora na Dodoma na kuwa huo ni mtandao uliotokana na michezo
hivyo inapaswa kuendelezwa.
Mwendo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza kwa mara nyingine kwa kutumia
maadhimisho hayo kuhamasisha sensa ya watu na makazi na kutoa faraja kwa Yatima
jambo ambalo wamekwenda mbali zaidi tofauti na malengo ya kufanya bonanza pekee
hivyo kumsaidia Rais Samia Suluhu
Hassan.
Pia Mwendo alisema kitendo cha kufanya maadhimisho hayo ni cha uungwana kwani wamejua umuhimu wake na
kitafungua milango na kwa wengine hasa wanaochipukia katika michezo.
Aliwataka washiriki wa bonanza hilo kucheza kwa kuzingatia kanuni na
taratibu zote za michezo na washiriki mchezo huo kwa usalama pasipo kuumizana.