Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manyoni na Itigi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Singida alioianza jana. Kutoka kulia waliokaa mbele ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Singida Jane Kessy, Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniphace, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Singida Dk.Denis Nyiraha na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo.
Na Dotto Mwaibale, Manyoni
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa,amewagiza Wakuu wa Wilaya wahakikishe
wanawasimamia Wakuu wa idara katika ukusanyaji wa mapato na utoaji wa huduma
kwa wananchi kwa kupanga muda wa kwenda kuwatembelea wananchi na kusikiliza
kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.
Ameyasema hayo jana Julai 15, 2022)
wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manyoni na Itigi akiwa katika
ziara ya kikazi mkoani Singida.
“Kila mmoja ahakikishe anatekeleza majukumu yake na kutoa taarifa kwa
wananchi juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika maeneo
yao,” alisema.
Majaliwa alisema alichobaini viongozi was Wilaya ya Manyoni hawaendi kwa wananchi kuwasikiliza
kero zao ndo maana kumakuwa na malalamiko mengi ya wananchi.
“Wakuu wa Idara hamuendi kwa
wananchi kusikiliza kero zao, hamuendi kuwaeleza mwelekeo wa Serikali yetu,”
alisema Mhe.Majaliwa.
Waziri Mkuu akisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia
Suluhu Hassan iko makini na haitaki mzaha katika matumizi ya fedha za umma
zinazoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema Serikali iko makini na rais alishatoa maelekezo kuwa hataki mzaha na matumizi ya fedha za
umma, hakuna atakayebaki salama na hakuna mtumishi atakayeonewa.
Alisema kuna wizi mkubwa wa mapato
ya Serikali kupitia mifumo ya makusanyo kwenye halmashauri nchini ikiwemo na
Halmashauri ya Manyoni.
Aliagiza kuwa kila aliyepewa dhamana ya kusimamia halmashauri ajipange
kusimamia makusanyo pamoja na matumizi yake.
Aidha,Waziri Mkuu amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida Bw. Mzalendo Widege kuwahoji wakusanya mapato
katika kituo cha mabasi cha Manyoni na katika mnada pamoja na Mkuu wa Idara ya
TEHAMA baada kubaini ufisadi.
“Makusanyo hayasimamiwi vizuri,
mfano katika kituo cha mabasi cha Manyoni Bw. Mussa Chacha ambaye si mtumishi
ila amepewa kazi ya kukusanya mapato hayo kwa mwezi Juni alipeleka benki
shilingi 1,786,000.”
Awali Waziri Mkuu aliweka jiwe la
msingi la ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Singida
inayojengwa katika kata ya Solya wilayani Manyoni na kupongeza uongozi wa
halmashauri hiyo kwa hatua iliyofikiwa. Shule hiyo ambayo itakapokamilika
itapunguza utoro na mimba kwa wanafunzi wa kike.
Akiwa njiani kuelekea Itigi kwa
ajili ya kuzungumza na watumishi wa umma, Waziri Mkuu alisimama Manyoni na
kusalimia wananchi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo suala
la machinga kutopangiwa maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao.
Malalamiko mengine yaliyotolewa na wananchi
hao ni pamoja na wajawazito kutozwa fedha pindi wanapokwenda katika hospitali
ya wilaya ya Manyoni kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za afya licha ya
Serikali kutoa huduma hizo za mama na mtoto bila ya malipo.