.
ASKOFU na Mwenyekiti wa
kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Dogo la Kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mussa
Nzumbi kulia akiteta jambo na Mchungaji wa Kanisa Waadventista Kana Tanga
Mchungaji wa Kanisa hilo Tanga Julius
Mbwambo kabla ya kuanza vikao vya maandalizi ya kuelekea
kusheherekea Jubilee ya miaka zaidi 50 ya Kanisa hilo
Na Oscar Assenga,TANGA.
ASKOFU na Mwenyekiti wa kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Dogo la
Kaskazini Mashariki mwa Tanzania Mussa Nzumbi amesema suala la Sensa ya
Watu na Makazi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi huku akieleza maana hata
bibilia inasema wana wa Israel walihesabiwa
Huku akiwahimiza
waumini wa kanisa hilo kuhakikisha wanashiriki kwenye zoezi la Sensa ya
Watu na Makazi kikamilifu ili Taifa liweza kujiua idadi ya watu na
kuweza kupanga mipango ya kuweza kuwahudumia.
Nzumbi aliyasema
hayo wakati wa vikao vya maandalizi ya Jubilee ya miaka 50 ya Kanisa
hilo katika kanda ya Tanga ambapo alisema wakati wanaelekea kwenye
maadhimisho hayo
Alisema sambamba na hilo wataendelea kuliombea
Taifa na viongozi ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwepo
ili wananchi waweze kupata nafasi ya kumuabudu Mungu.
Alisema
kuelekea Jubilee hiyo wanamshukuru Mungu amewasaidia kwenye eneo hilo
wamekuwa na ongezako kubwa la waumini na huduma za kijamii ikiwemo shule
ya Kana Central English Medium na wamekuwa na huduma za kijamii
wanazofanya maeneo mbalimbali kama kutoa damu hivyo yote yanawaleta
pamoja kutafaraka.
Aidha alisema wanaendelea kuhimiza suala la
sensa ya watu na makazi kwa maana suala hilo ni la kibibilia hata wana
wa Israel walihisabiwa hivyo ni muhimu kwa sababu ili taifa liweza kujua
idadi na serikali iweze kuwahudumia.
“Kwenye Jubilee hii
tunaiombea Serikali,wananchi Mungu aendelee kutulinda amani na upendo
vikatawale kwenye Taifa letu tunaamini kunapokuwa na utulivu ndio
tunapata nafasi ya kwenda kumuambudu mungu kwa uhuru na utulivu
zaidi”Alisema Askofu Nzumbi
Hata hivyo alisema kwamba wanaiombea
pia Rais ,Serikali ,Mkoa wa Tanga na maeneo mbalimbali yaweze kuwa
salama na amani iweze kutawala .
“Tupo hapa Kanda ya Central kwa
ajili ya mikutano ya Jubilee ya miaka 50 ya Kanisa hilo Jijini Tanga
tunamshukuru Mungu ametusaidia kazi kwenye eneo hilo tumekuwa na
ongezako kubwa la waumini na huduma za kijamii kama shule ya Kana
Central English Medium na wamekuwa na huduma za kijamii tulizofanya
maeneo mbalimbali kama kutoa damu yote hayo yanawaleta pamoja
kutafarakani”Alisema
Akofu Nzumbi alisema wana mshukuru Mungu
kwa kazi kubwa na Jubilee hiyo inawasaidia wa waumini watafakari mahali
walipotoka na mahali wanapokwenda.
“Lakini tuna mikakati kufungua shule ya sekondari Ngomeni itakayosaidia vijana wetu waweze kupata elimu ya dunia sambamba na kufungua kituo vya afya kwenye baadhi ya maeneneo nitoe wito kwa Jamii,kanisa na wananchi tuendelee kushiriki kwa mshikamano tufanye kazi tuendelea kusaidiana”Alisema Askofu Nzumbi
Naye kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Wasabato Julius Mbwambo alisema tukio la kusheherekea maiaka zaidi ya 50 katika kanda ya Tanga ni kazi
ya mungu imekuwa sana na kwa miaka hiyo wanakiri kumuona mungu akitembea nao.
Alisema wanaendelea kusherehekea miaka ya kazi ya Mungu
na wanaamini yule Mungu aliyekuwepo hapo awali waendelea kuwa naye huku
akieleza wataendelea kuifanya kazi ya Mungu mpaka atakaporudi kwa mara
ya pili .