Na Mwandishi wetu, Handeni
Wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) imeleta faraja Kwa wakazi 17,000 wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga Kwa kuwapata maji safi na Maji ya Mifugo .
RUWASA inatumia zaidi ya sh 3 bilioni Kwa sasa katika miradi ya maji Msomera Kwa kusambaza maji na kichimba bwawa kubwa la Mifugo.
Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA,Mhandisi Clement Kivegalo akizungumza na waandishi wakati wa kutembelea kijiji Cha Msomera kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika eneo hilo, amesema hadi kufikia mwakani kijiji hicho kitakuwa cha mfano kupata maji safi na salama.
Mhandisi Kivegalo amesema hadi sasa utekelezwaji miradi ya maji Msomera imefikia zaidi ya asilimia 80, ambapo visima vitatu virefu vimechimbwa na vinatoa Maji zaidi ya lita 775,000 na mahitaji yote ni lita 450,000.
Amesema pia RUWASA inaendelea na mradi wa kuchimbwa bwawa ambalo litakuwa na Maji lita milioni 725 ambazo zitatumiwa na Mifugo na binaadamu..
Meneja RUWASA mkoa wa Tanga, Upendo Omary amesema katika mradi huo hadi sasa Bomba zenye urefu wa kilomita 14 tayari zimechimbiwa chini na lengo kusambaa kilomita 20.8.
Amesema katika mradi huo tayari matanki yamendaliwa na baadhi yameanza kupokea maji kuna Tanki lita 10,000 na jingine lita 167,000 na kutakuwa na vituo 24 vya kutoa maji.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Handeni, Hosea Joseph amesema watu 17,000 watanufaika na mradi huo wakiwepo watu 6,036 ambao ni wenyeji wa Kijiji hicho.
Amesema Bwawa katika Kijiji hicho litakamilika May 2023 lakini pia kuna mradi wa kujenga maeneo ya mifugo kunywa maji ambayo yatakamilika karibuni.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Msomera , Martin Ole Ikayo alipongeza Serikali na Rais Samia Suluhu kwa msaada mkubwa uliotolewa kwa Kijiji hicho.
“Sisi tunapongeza sana Rais Samia Suluhukwa maendeleo makubwa katika Kijiji chetu na uamuzi kuletwa wananchi wa Ngorongoro Msomera leo tuna shule, Sekondari na msingi , Kituo cha afya ,tuna umeme na Maji”amesema
Ikayo amesema shida ya Maji katika Kijiji imekwisha na sasa maji yameanza kutoka na hadi nyumbani kwake na RUWASA imefanya kazi kubwa sana katika Kijiji hicho.
Kijiji Cha Msomera kinaendelea kupokea wananchi ambao wanachama kwa hiari katika eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.