Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Profesa Godius Kahyarara (kulia) akiwa na Meneja Sekta Isiyo Rasmi Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Rehema Chuma wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam Julai 10, 2022. NSSF imewekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi mbalimbali hapa nchini.
“kama mnavyojua NSSF ni moja ya taasisi kubwa hapa nchini zinazowekeza kwa kiasi kikubwa sana, tunatumia nafasi hii kutangaza uwekezaji wetu nyumba zetu za kupangisha na kununua mfano tuna nyumba huko Wilayani Kigamboni hususan Mtoni Kijichi, Tuangoma, Dungu, maeneo ya Muongozo.
Tuna nyumba nzuri sana na mwitikio wa kununua nyumba hizo umekua ni mzuri sana, pia tunajenga jengo la Mzizima hapa Dar es Salaam na nia hasa ni kulipangisha kwa watu watakaoendesha mradi wa hoteli pia Mwanza na lengo ni hilo hilo kulipangisha kwa mtu atakayeendesha shughuli za hoteli, tunatumia Maonesho haya kutangaza hizo nafasi ndani ya nchi lakini pia nje ya nchi ili tuweze kupata wadau hao ili kuhakikisha tunapata wapangaji au kununua nyumba hizo.” Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Masha Mshomba aliwaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa Maonesho hayo wiki iliyopita.
Profesa Kahyarara akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa IT Nuru Mbeyu kuhusu huduma za TEHAMA.
Profesa Kahyarara akipata maelezo kuhusu uwekezaji.
Profesa Kahyarara akizungumza jambo wakati akiwa na Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi NSSF Bi. Rehema Chuma (kushoto) na Meneja wa Mkoa wa TEMEKE NSSF, Bw. Feruzi Mtika.