****************************
NA BALTAZAR MASHAKA,Ilemela
DIWANI wa Kiseke (CCM) Manispaa ya Ilemela,Ramadhan Mwevi,leo amewaongoza wazazi na uongozi wa shule ya sekondari ya Angelina Mabula,kuweka mikakati ya kutokomeza daraja sifuri kwa kuboresha taaluma na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Mikakati hiyo ni kuanzisha masomo ya ziada,kuajiri walimu nje ya mfumo,wazazi kuchangia fedha waliyokubaliana katika vikao na kupata kibali, kuboresha darasa moja kuwa maabara ya muda, kuongeza vifaa vya maabara,kufanya mitihani na majaribio ya mara kwa mara na motisha kwa walimu.
Mwevi akizungumza katika mkutano wa wazazi shuleni hapo leo,amesema shule hiyo inaweza kuwa ya kwanza wilayani Ilemela katika mitihani ,hivyo ni lazima iungwe mkono isonge mbele kwa watoto kupata matokeo mazuri ya kitaaluma endapo mikakati hiyo itatekelezwa.
“Jiwe la pembeni lililokataliwa na waashi limeanza mambo, tunatamani kuona Angelina Mabula sekondari mpya yenye matokeo bora ya taaluma,hivyo tuache kusinzia,tujitoe na tulipeni michango tuliyokubaliana,tunahitaji milioni 9.8 za kuanzia, ”amesema
Mwevi alichangia sh. 500,000 za ujenzi wa kantini na hosteli ya wasichana,ununuzi tenki la maji na mashine ya kudurufu maandishi,aliwataka wazazi wa eneo hilo kuwa na dhamira itakayoifanya Angeline sekondari kufanya vizuri kitaaluma baada ya maboresho kufanyika.
“Nilipata hofu baada ya kubadilishwa mkuu wa shule,leo matokeo yameanza kuonekana,watoto waliokimbia mitihani bila sababu bodi itaweka adhabu kudhibiti changamoto hiyo,”alisema kabla ya kuchangia sh.milioni 1,000,000.
Mwijage amewasistiza wazazi kuwa ndio dira ya bodi,hivyo watimize wanayokubaliana katika vikao kwa maendeleo ya elimu,ukuaji wa taaluma kwa watoto na shule yenyewe,kwani kipimo cha mkuu wa shule ni matokeo na bila hivyo watamweka pagumu.
Baadhi ya wazazi wamesema wengi hawaoni umuhimu wa elimu ya watoto wao ndio sababu wanaoona vigumu kuchangia sh.2000 za taaluma kwa mwezi na sh.5,000 za kununua mashine ya kudurufu maandishi na kushauri wasiingize siasa katika elimu ya watoto wao.
Mmoja wa wazazi hao Lazaro Katula,amesema mkuu wa shule ana maono na ubunifu wa taaluma unaolenga kutokomeza daraja sifuri pia malezi ni sadaka kubwa kwa watoto na kuwashauri wazazi kumkumbatia na kumficha ili aendelee kushirikiana na walimu waliopo na kuwajengea uwezo wa kitaaluma.
“Tunapiga kelele kupata walimu wakiwemo wa ziada kukidhi mahitaji ,hivi tukiendelea hivi bila kulipa sh.2,000 tutapata watoto waliolelimika sawa na watoto wa walionacho,”amehoji Katula.
Aidha Winfirda Alex alionyeshwa na baadhi ya wazazi kushindwa kuchangia taaluma ya watoto wao na kushauri majina yao yaorodheshwe na kufikishwa kwa mtendaji wa kata sababu michango hiyo wamekubaliana na kupata kibali kma unavyoelekeza waraka wa elimu namba 3/2016 na namba 6/2016.
“Tusiweke siasa katika elimu vinginevyo tutakwama na tutambebesha mzigo na lawama mkuu wa shule maana haya wazazi tulikubaliana katika vikao,” amesema mmoj wa wazazi aliyfahamika kwa jina moja la Kuzenza.
David Misase amesema kuwa mkuu wa shule anafanya kazi kubwa ya kujenga taaluma ya watoto ili kupindua matokeo kwa kuongeza ufaulu,hivyo wazazi na jamii waache ngonjera watimize wajibu wao kwa maendeleo ya taaluma ya watoto vinginevyo watafanyiziana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi, Kamani Shigela amesema mchakato wa ujenzi hosteli na kantini umeanza,lengo ni kufanisha maendeleo na kuinua taaluma ya watoto,wakati ukiendelea waangalie pia bweni la wavulana maana ipo faida watoto kusoma wakiwa bwenini.