************************
Na Mwandishi wetu, Manyara
TAASISI ya Ihsani Foundation ya jijini Arusha kwa kushirikiana na IDDEF ya nchini Uturuki wametoa msaada wa nyama ya mbuzi 850 na ng’ombe 150 kwa wajane, yatima na wasiojiweza wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Katibu wa taasisi ya Ihsani Foundation ya jijini Arusha, ustaadhi Abdul Ally amesema nyama ya mifugo hiyo inatolewa kwa wahitaji hao wakiwemo wajane, yatima na wasiojiweza.
Ustaadhi Abdul amesema nyama za mifugo hiyo zimetolewa kwa ufadhili wa taasisi ya IDDEF ya Uturuki.
Amesema katika kusherehekea Idd el haji nyama za mifugo hiyo zimetolewa kwa wahitaji mbalimbali hao bila kujali itikadi ya dini.
Amesema ili kusherehekea sikukuu hiyo wamegawa nyama ya mifugo hiyo ikiwemo mbuzi, ng’ombe 150.
Hata hivyo, amesema taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo shule, mahabusu na vituo vya watoto yatima wamepatiwa nyama hizo.