p>
“Mhe Mgeni Rasmi kutokana na changamoto hizo nilianza
kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha napunguza au kuondoa changamoto hizo
kabisa”
“Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kupeleka maswali na hoja
zinazohusu watu wenye Ulemavu Bungeni ili kutafuta ufumbuzi ikiwemo mabadiliko ya
kisheria na sera mbalimbali kuendana na mazingira yao”
“Hatua nyingine niliamua kuanzisha kampeni maalum ya
kusaidia vifaa saidizi ikiwemo fimbo, basikeli, mafuta na hata kuboresha
miundombinu katika baadhi ya maeneo ili wasikutane na changamoto hiyo” amesema Mhe. Kabati.
Aidha, ameongeza kuwa baada ya kuona hali ya uhitaji katika jamii
ni kubwa, aliamua kuanzisha Taasisi maalum ya kushughulikia changamoto zinazowakabili watu waliopo kwenye makundi maalum inayoitwa RITTA KABATI TRUST FUND, ambayo itajihusisha moja kwa moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto za watu wenye mahitaji maalum kwa kuwafuata kwenye maeneo yao na kuwatambua ili kufanya uratibu wa kuwasaidia.
“Taasisi hii inalenga Kukuza utu na heshima kwa watu wenye ulemavu na kutoa
ushauri wa matibabu bila malipo kwa walemavu pamoaja na kusaidia miradi na shughuli nyingine
za kiuchumi zinazoendeshwa na watu wenye ulemavu” ameongeza Mhe. Kabati.
Aidha amebainisha kuwa kazi nyingine ni kuanzisha na kudumisha vituo vya walemavu ili kusaidia
jamii na kujihusisha katika michezo hususani ya watu wenye ulemavu kwa kuanzisha mashindano mbalimbali ya michezo na burudani katika Mkoa wa Iringa.
Kazi nyingine ni pamoja na kusaidia programu na mipango inayolenga kuwaelimisha na kwafahamisha wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu kuhusu changamoto mahususi zinazowakabili watoto wenye ulemavu na jinsi ya kuwatunza.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amempongeza Mbunge Kabati kwa hatua yake ya kusaidia watu wenye mahitaji maalum na kwamba kwa kufanya hivyo anaunga mkono jitihada za Serkali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vya ukatili hasa kwa watoto na walemavu.
Sendiga amsema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Mkoa huo unaongoza kwa ukatili wa kijinsia na kwamba jamii yote hususani wakazi wa Mkoa huo wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kutokomeza vitendo hivyo kama anavyofanya Mbunge Kabati.
“Ni aibu sana na fedheha kwa mkoa wetu kuongoza katika vitendo vya ukatili wa kijinsia, tunapaswa kupiga vita kwa nguvu zetu zote na mtu akikutwa na hatia ya kuhusishwa na vitendo hivi anapaswa kuchukuliwa hatua kali hata kufungwa maisha” amsema Mkuu wa Mkoa huyo huku akionesha kukasirishwa na vitendo hivyo.
katika hatua nyingine amezungumzia umuhimu wa watu wenye ulemavu kushiriki katika Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Ogasti mwaka huu na kuhimiza kuhesabiwa kwa watu wenye ulemavu na kwamba zoezi hilo litaifanya Serikali kutambua idadi ya watu hao na hivyo kupata huduma kwa urahisi kutokana na mahitaji yao na maeneo walipo.
“Ndugu zangu naomba sana kuhamasisha wazazi na walezi kuhakikisha watu wote wenye ulemavu tulinao majumbani wanahesabiwa, usimfiche mtu mwenye ulemavu kwani kwa kufanya hivyo utaifanya Serikali kukosa idadi yao na hivyo kushindwa kuwafikia kuwapatia huduma zao wanazostahili” amesisitiza RC Sendinga.
MATUKIO KATIKA PICHA MBALIMBALI ZA MAANDAMANO