Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius Maneno, akipata elimu kuhusu masuala ya bajeti ya Serikali, kwa Mhasibu Bi. Agneth Rushekya kutoka Wizara ya Fedha na Mipango alipotembelea Banda la Wizara katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, jijini Dar es Salaam. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Mchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Eliasi Masanza akimuonesha kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2022/23 Bi. Gladness Godfrey, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, jijini Dar es Salaam. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius Maneno, akisikiliza maelezo kuhusu sera kutoka kwa Mchumi Bw. Johnpaul Kisombo alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Mchumi Idara ya Usimamizi wa Madeni kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Sepo Seni, akitoa elimu kuhusu deni la Taifa kwa Bw. Ahmed Hilel, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Mchumi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Gibson Sabayo, akisikiliza maoni kutoka kwa Bi. Grace Naburi alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)