Mtu mmoja ambaye hajajulikana akionekana ndani ya ofisi ya Shirika la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) lililopo katika Manispaa ya Singida mkoani hapa baada ya kuvunja milango na kuiba fedha taslimu pamoja na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. 7,760,000.
Mtu huyo akiwa ndani ya ofisi za shirika hilo akiketeleza wizi.
Mtu huyo akiwa ndani ya moja ya chumba cha ofisi hiyo akitekeleza wizi.
Mtu huyo akiingia katika ofisi hizo kwa ajili ya kufanya wizi.
Mtu huyo akiwa ndani ya ofisi ya shirika hilo akivunja dirisha ili aingie ndani.
Mtu huyo akijifisha kwa mkono wake ili kamaera za usalama zisiweze kuninasa sura yake.
Mtu huyo akifanya uhalifu ndani ya ofisi hiyo.
Mtu huyo akiwa ndani ya ofisi hizo.
Mtu huyo akiwa ndani ya ofisi hizo.
Mtu huyo akiwa ndani ya ofisi hizo.
Thobias Mwanakatwe na Dotto Mwaibale, Singida.
MTU mmoja ambaye hajajulikana amevunja milango na kuiba fedha taslimu pamoja na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. 7,760,000 mali ya Shirika la Jiokoe na Umaskini yaani Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) lililopo katika Manispaa ya Singida mkoani hapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Dk. Suleiman Muttani, akizungumza na waandishi wa habari alisema tukio hilo limetokea Juni 26 mwaka huu kati ya Saa 11:30 na saa 12:00 jioni katika ofisi hizo zilizopo kati ya ofisi za mkoa za kampuni ya simu ya Tigo na Shirika la Ugavi Umeme (TANESCO) Kata ya Ipembe Manispaa ya Singida.
Alisema taarifa za tukio hilo ambalo mtuhumiwa alinaswa na camera za CCTV wakati akiiba, limeripotiwa katika kituo cha polisi Singida Kati na kusajiriwa kwa namba SGD/IR/3240/2022.
Dk.Muttani alitaja vitu vilivyoibwa kuwa ni kompyuta mpakato ( Laptop) aina ya HP, TV inchi 36, Projector Epson, Hard disc mbili zenye ukubwa wa GB 500 na GB 1000 pamoja na fedha taslimu Sh.2,000,000 ambazo zilikuwa zimewekwa ofisini kwa ajili ya kulipia pango la ofisi.
Dk.Muttani alisema mwizi huyo ambaye ameonekana na CCTV Camera akiwa amevaa kofia, shati jekundu, koti jeusi na suruali nyeusi katika ya kuiba alivunja milango mitano ambayo ni wa kuingilia getini, kliniki na ofisi za utawala za SPRF.
Aliongeza kuwa mwizi huyo wakati akifanikisha uhalifu huo alinyofoa ya baadhi ya camera za CCTV lakini nyingine zilizobaki ambazo hakuziona ziliweza kumnasa wakati akitekeleza wizi huo.
“Mwizi huyo baada ya kufanikisha uhaliifu huo alichukua funguo za ofisi na kuzipanga juu ya viti ambavyo wanaketi watu wanapokuja kufuata huduma za matibabu,” alisema.