Sehemu ya ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea
Mbunge
wa Pangani (CCM) na Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika akitembelea
ujenzi huo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Hassan
Nyange kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo
NA OSCAR ASSENGA, PANGANI.
MBUNGE
wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa
kufanikisha ujenzi wa Barabara ya kutoka Tanga-Pangani –Saadan huku
akieleza kwamba utawala wake umekuwa ni suluhu ya matatizo ya watanzania
na wana Pangani .
Amesema ujenzi wa barabara hiyo
utakapokamilika utalifungua jimbo hilo kiuchumi na hivyo kusaidia
wananchi kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kimaendeleo kutokana na
uwepo wake.
Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji aliyasema hayo
leo wakati wa ziara yake ya kukagua na kutembelea ujenzi wa barabara ya
Tanga –Pangani-Bagamoyo kwa kiwango cha lami lenye kilomita 256.
Huku
akiridhishwa na kasi ya utekelezaji wake unavyokwenda huku akiwahaidi
ushirikiano wakandarasi wanaotekeleza mradi huo ili kuhakikisha ujenzi
huo unakwenda kama ulivyopangwa.
Alisema kwa sababu wilaya ya
Pangani walikuwa na na changamoto ya barabara na wapo ambao walikuwa
hawaamini kwamba ujenzi huo utafanyia lakini leo ujenzi unaendelea.
“Wapo
ambao walikuwa hawaamini kwamba ujenzi wa barabara hii utajengwa lakini
leo hii hapa inajengwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu
tunamshukuru sana kwa hili kubwa alilotufanyia sisi wana Pangani”Alisema
Mbunge Aweso.
Aidha aliwataka wana Pangani wachangamkie fursa
za ujenzi wa mradi huo wa barabara kwa kuongeza uzalishaji zaidi kwa
kutumia ardhi iliyopo kwa ajili ya kilimo ikiwemo kuwataka kuacha kuuza
maeneo yao kiholela,
“Niwaombeni ndugu zangu sasa ujenzi huu
unafanyika hii ni fursa na maendeleo kwa sababu itafungua fursa za
kiuchumi hivyo niwasihi acheni kuuza ardhi kiholela holela kwa
kuhakikisha mnayasimamia kutokana na fursa za kiuchumi zitafunguka
wakati ujenzi huu utakapokamilika na kuweza kupata maendeleo”Alisema
Alisema
kwa sababu ujenzi wa barabara hiyo unakwenda kuitoa Pangani pangoni na
kuiinua kiuchumi na hivyo kufungua fursa za kimaendeleo hivyo wananchi
hakikisheni mnaongeza uzalishaji.
“Niliwahi kupiga magoti hapa
kuomba barabara hii lakini naishukuru Serikali inayoongozwa na Rais
Samia kwa kutufuta machozi wana Pangani kwa kuliona hili na utekelezaji
wa mradi huu kwa sasa unaendelea na kubwa zaidi unakwenda pamoja”Alisema
“Nimeanza kukagua eneo la Choba nimeridhika sana na utekelezaji
wake nifikisheni salamu za pongezi kwa Waziri wa Ujenzi Profesa Makame
Mbarawa na Watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) kwa kuwapata
wakandarasi wazuri wanafanya kazi vizuri”Alisema
Aliongeza yeye
kama mbunge wa Jimbo la Pangani aliwahaidi wakandarasi hao kwamba
watawapa ushirikiano kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati huku
akiwaeleza kwamba changamoto ambazo aliwaeleza atakwenda kukutana na
Waziri wa Ujenzi kuona namna ya kuzipatia suluhu”alisema
Hata
hivyo aliwapongeza Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) mkoa wa Tanga
kutokana na kwamba wanafanya kazi nzuri hasa juu ya usimamizi na
ufuatiliaji wa mradi huu.
“Rais Samia ni Rais wa nchi nzima
lakini ametambua kiu ya wananchi wa Pangani miaka ya nyuma ukitaka
kwenda Pangani kutoka Tanga unacheza kiduku mpaka unafika Pangani
kutokana na miundombinu mibovu ya barabara lakini ujenzi huo utaondosha
changamoto hizo”Alisema.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) Mhandisi Zuhuru
Amani alisema ujenzi wa barabara ya Tanga –Pangani kilomita 50
uligharimu kiasi cha Sh. bilioni 66.853 ambayo ilikuwa ni gharama za
awali lakini imeongezeka na sasa kuwa Bilioni 67.458 kutokana na
mabadiliko ya usanifu,
Mradi huu ulipangwa kukamilika Novemba 14
mwaka 2021 lakini kutokana na sababu mbalimbali za kimkataba mufa wa
kukamilika kwa mradi huo umeongezwa hadi Desemba 5,2022 na kazi hiyo
inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.
Alisema
mradi huo mwanzoni ulikuwa ukisimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S TECU
(TANROADS Engineering Consulting Unit) hadi Desemba 5 mwaka 2020 na kwa
sasa unasimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S Dotch LTD ya Tanzania kwa
gharama ya Sh.Bilioni 2.246 na utekelezaji wa mradi huo umefikia
asilimai 42.3 na hadi sasa mkandarasi amelipwa hati nne za madai zenye
jumla ya Sh.Milioni 8,
Alisema awamu ya pili ya mradi huo ni
ujenzi wa daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525 utahusisha
ujenzi wa barabara ya maungio ya daraja yenye kilomita 14.3,barabara ya
mchepuko ya kwenda ushongo kilomita 5.9 na barabara za Pangani mjini
zenye urefu wa kilomita 5.4.
Mhandisi Zuhura alisema mradi huo
unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkataba
umesainiwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroad) na
Mkandarasi M/s Shandong Luqiao Group Co.Ltd kutoka Chini Mei 5 mwaka huu
kwa gharama zaidi Sh. Bilioni 82 kwa muda wa miezi 36 ya ujenzi na
miezi 36 ya kipindi cha uangalizi kwa upande wa daraja ni miezi 12 kwa
upande wa barabara.
Hata hivyo alisema kwa upande wa barabara ya
Tungamaa –Mkwaja-Mkange kwa kiwango cha Lami (Km 95.2) ikijumuisha na
barabara ya mchepuko ya Kipumbwi yenye kilomita 3.7 unafadhiliwa na
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mradi huo ulishasainiwa na
mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchini.
Alisema na
mkandarasi M/s China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G) kutoka
china kwa gharama za zaidi ya Sh.Bilioni 94 na kwa sasa muda wa miezi
36 ya ujnzi na miezi 12 ya kipindi cha uangalizi na kazi ya ujenzi
imeanza Aprili Mosi mwaka huu na inatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 31
2025 na zaidi ya Bilioni 14 zimelipwa kwa mkandarasi na mpaka sasa
ikiwa ni malipo ya awali ya Mhandisi Mshauri kuidhinisha malipo hayo na
utekelezaji wake umefikia asilimia 5.1.