Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wananchi wa kijiji cha Namapuya wilayani Nachingwea baada ya kukagua mashamba yao yaliyoharibiwa na tembo waliovamia kijiji hicho, Julai 6, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandila wilayani Nachingwea wakati alipotoa pole kwa wananchi hao ambao vijiji vyao vilivamiwa na tembo waliosababisha kifo cha mtu mmoja, Riziki Rashid Issa na kuharibu mashamba ya mazao ya chakula katika baadhi ya vijiji wilayani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)