Naibu waziri wa elimu ,Omari Kipanga akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha .
Naibu waziri wa elimu ,Omari Kipanga akizindua rasmi shule jumuishi ya mfano ya sekondari Patandi iliyopo Tengeru mkoani Arusha.
************************
Jackline Laizer,Arusha.
Arusha.Naibu waziri wa elimu, Omari kipanga amesema kuwa,serikali ya awamu ya sita imeendelea kuweka msukumo mkubwa katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizindua shule jumuishi ya mfano ya sekondari Patandi iliyopo Tengeru mkoani Arusha iliyojengwa na wizara ya elimu Sayansi na teknolojia kupitia mradi wa lipa kutokana na matokeo ya Ep4R .
Kipanga alibainisha mambo yaliyowezeshwa na Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu yakiwemo ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu mbali mbali ambayo ni rafiki na sikivu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika ngazi zote za elimu ya awali sekondari na vyuo pamoja na ununuzi , usambazaji wa vifaa vya kujifunzia na kujifunzia pamoja na vifaa saidizi vya kisasa na kidigitali kama vile bajaji , will chear , kompyuta na viti.
Aidha ametoa rai kwa familia na wadau wa maendeleo kuendelea kuchangia juhudi za serikali katika kuwapatia huduma stahiki wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika mchango mzima wa kujifunza .
Aidha amewataka wazazi waone umuhimu wa kuwaandikisha watoto wenye uhitaji maalumu katika Shule zilizopo jirani ili nao waweze kupata haki zao za msingi za walivyo watoto wengine.
Kwa upande wa Mkuu wa Shule jumuishi ya mfano wa sekondari Patandi, Jannet Mollel amesema watoto wote wana fursa sawa bila kujali changamoto zao huku akiishukuru serikali ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Raisi Samia suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kujenga Shule hiyo kwani imekuwa mkombozi kwa watoto wenye mahitaji maalumu.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru , Mhandisi Richard Ruyango ameishukuru Serikali kwa kujenga shule hiyo katika wilaya ya Arumeru na kutoa wito kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalumu kuwafikisha katika shule hiyo ili waweze kujifunza na kusoma pamoja na kuhitimu vizuri na kuwataka walimu na wakufunzi kuwatunza na kuwajali wanafunzi hao pamoja na kutunza miundo mbinu ya majengo ya Shule hiyo.
Aidha shule jumuishi ya mfano ya sekondari Patandi ni ya kwanza nchini kuwa na miundombinu stahiki kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na imegharaimu zaidi ya shilingi bilioni 3.8 .
Hata hivyo Shule hiyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 400 na mpaka Sasa ina idadi ya wanafunzi 288 wakiwemo wanafunzi viziwi 144 , wasio ona 1, Uoni hafifu 6, viziwi na wasio ona 3, wenye ulemavu wa viungo 51, wenye ualbino 9 ,Wenye usonji 1, Wenye ulemavu wa akili 2 , na wasio na ulemavu 71.