MWANAFUNZI wa darasa la 6 kutoka katika shule ya msingi Isuna Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Rosemary Masaka akiwa ameshikilia cheti na zawadi ya shilingi 400,000/baada ya kushinda uandishi wa Insha
Baadhi wa wazazi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutika shule mbalimbali katika mkoa wa Tabora aliyevaa kafia na tisheti nyekundu kifuani ni Saimon Masaka baba mzazi wa Rosemary Masaka
***************************
Na Lucas Raphael,Tabora
MWANAFUNZI wa darasa la 6 kutoka katika shule ya msingi Isuna Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Rosemary Masaka ameibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza katika umahiri wa kuandika Insha inayohusu kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Akizungumza katika halfa hiyo mratibu wa mpango wa maendeleo ya Jamii wa shirika la World Vision Tanzania,Clasta ya Nzega mkoani Tabora Michael Ngasa alisema kwamba mchakato wa kuwapata wanafunzi hao ulifuata sheria na kanuni zote ziliweka na shirika hilo.
Alisema kwamba shirika ndilo liloratibiwa shindano hilo la kuandika Insha ambalo liliusisha wanafunzi wa madarasa ya sita na saba kutoka katika Wilaya ya Nzega ,Igunga na Uyui na kilele chake kumalizika katika kata ya Puge iliyopo Wilaya ya Nzega ,Washindi wa Insha hiyo walikabidhiwa na shirika hilo zawadi za baiskeli na fedha tasilimu kwa washindi wa ngazi za Wilaya ya Mkoa .
Meneja wa shirika la World Vision Tanzania wa kanda ya shinyanga ,Simiyo na Tabora Jaegueline Kahaura alisema kwamba Mwanafunzi Rosemary Masaka aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa uandishi wa Insha katika Mkoa wa Tabora kwa kuandika kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Alisema kwamba lengo la shirika ni kuwajengea uwezo watoto wa kujiamini na kujitambua ikiwa hatua ya kukabiliana na tatizo la mimba na ndoa za utotoni .
Alisema kwamba shirika hilo litaendelea kuratibu mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo washindi wamepewa zawadi za baiskeli na fedha tasilimu huku mshindi wa kwanza kwa mkoa wa Tabora akitarajiwa hivi karibuni kwenda kushiriki mashindano hayo kitaifa Mkoani Dodoma.
Nae Mwanafunzi wa darasa la 6 kutoka katika shule ya msingi Isuna Rosemary Masaka aliamua kuandika maudhui yanayohusu kupinga mimba na ndoa za utotoni kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo katika Mkoa wa Tabora huku akiiomba serikali kuongeza makali katika kusimamia sheria zinazolinda haki za mtoto.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega kamishina msaidizi wa polisi Advera Bulimba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora balozi Dkt. Batilda Burani katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao na kuwapongeza washiriki wa shindano hilo amesema serikali haina lelemama kwa wale wanaovunja matakwa ya haki za watoto.