Mkurugenzi wa Lake Oil Group, Ally Edha Awadh mara baada ya kupokea Tuzo ya Mfanyabiashara Kijana kwa mwaka 2022 katika bara la Afrika.
***************************
Mkurugenzi wa Lake Oil Group, Ally Edha Awadh jana amepokea Tuzo ya Mfanyabiashara Kijana kwa mwaka 2022 kwa Afrika nzima.
Tuzo hiyo alipokea jana nchini London, Uingereza baada ya kuwashinda wapinzani wake watatu, Sangu Delle, ambaye ni Mwenyekiti wa kampuni ya Golden Palm Investments Corporation ya nchini Ghana.
Wengine ni Stephen Sembuya, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Pink Foods Industries ya Uganda na Emmanuel Ademola Ayilara, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya LandWey Investment Limited ya nchini Nigeria.
Awadh ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo iliyojikita kweye biashara ya mafuta na gesi, amekabidhiwa tuzo hiyo Jana kwenye Ukumbi wa House of Lords jijini London, Uingereza ambazo ni miongoni mwa kumbi maarufu zaidi duniani.Tuzo hizo zinazotolewa na Jarida la African Leadership.
Lake Oil imejikita zaidi katika biashara ya vituo vya kuuza mafuta kwenye maeneo mbalimbali nchini sambamba na gesi zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani.
Mbali na hilo, Awadh anatajwa kama mfano kwa vijana ambapo, kupitia kampuni zake hizo amesaidia kutoa ajira kwa makundi ya vijana huku ufanisi wa kampuni hizo ukichukuliwa kama mfano bora kwa vijana kuendesha biashara kwa tija.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Lake Oil alisema ilikuwa kumbukumbu ambayo hataisahau kwa maisha yake yote.
“Nilikabidhiwa Tuzo ya Kiongozi wa Biashara Vijana barani Afrika katika Jumba la Mabwana Mashuhuri hapa London, mbali ya faraja kwangu lakini nimefurahi zaidi tuzo hii kupatikana kwa kijana wa Kitanzania,” alisema Bw.Awadh.
“Natoa shukrani zangu za dhati kwa Mama na Baba yangu kwa Sala na Baraka zao zisizo na mwisho, familia yangu, haswa Mke wangu, kwa nyakati zote ambazo nimekuwa mbali na kuzingatia biashara zetu,” alisema Awadhi.
Pia alitoa shukrani kwa timu nzima ya wafanyakazi wa makampuni ya Lake Oil sehemu mbalimbali Afrika zilipo ofisi zake na mwisho kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwapa nguvu za kufanya kazi na kutimiza malengo yao.
Edha ambae miaka ishirini na miwili (22) iliyopita aliweza kupata mapato yake mwenyewe akifanya kazi kwenye mgahawa wa Mac Donald wakati akisoma shahada yake yake ya kwanza huko Canada.
Aliporudi nchini kutoka masomoni alianza ujasiliamali kuanzisha biashara yake ya kwanza ya kuuza mitumba kutoka Canada hadi Tanzania. Nilijijengea mtaji na kuanzisha tawi la kuagiza lori zilizofanyiwa ukarabati kutoka Uingereza hadi Tanzania.
“Muda si muda nilikuwa milionea kijana nikiwa na umri wa miaka 26 tu.Nilifurahishwa sana nilipoenda kwa Wakala wa Ununuzi wa Mafuta kwa Pamoja nchini Tanzania nikiwa na Ofisi yangu ya Biashara ili kupata leseni ya Uagizaji wa Petroli” Alisema Bw. Awadhi akitoa ushuhuda wake mbele ya wafanyabishara wenzake.
Alitimiliza mahitaji yote ambayo yalimwezesha kuwa kati ya wafanyabiashara wakuu. Ilikuwa mwaka 2006 ambapo Lake Oil ilizaliwa na baada ya kupata leseni iliyobaki imekuwa historia nzuri kwake na pia kwa nchi yake Tanzania.
Tangu wakati huo nimeongeza biashara yangu sio katika mafuta pekee bali hata katika uwekezaji wa viwanda. Pia nimeendelea kuwekeza katika nchi nyingine na kuacha alama katika nchi hizo kama muwekezaji kutoka Tanzania.
Aliwaomba washiriki wa tuzo hiyo, wasiruhusu hadithi yake nzuri ya mafanikio iwadanganye, wamekumbana na changamoto kadhaa kwa miaka mingi, ikiwa ni pamoja na Kimbunga Idai ambacho kilikumba na kuteketeza ghala kubwa ya kuhifadhia mafuta alioijenga nchini Msumbiji mwaka wa 2019.
Baada ya miezi 9 moto ulizuka katika Ghala ya kuhifadhia mafuta lake Oil makao makuu kigamboni Dar es Salaam na kusababisha uharibifu na hasara kubwa. Sekta yetu ni tete na kwa haraka mabilioni yanaweza kupotea.
Janga la Covid-19 ilitufunza ustahimilivu mkubwa katika biashara. Tulijifunza, hata bidhaa ya thamani kubwa haina thamani wakati hakuna Mahitaji. Hata hivyo, ujumbe wangu hapa ni kwamba unaweza kupitia kila aina ya vikwazo maishani.