Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
BWENI la Wavulana Chalinze Modern Islamic Primary School , Mkoani Pwani la ungua Moto ,alfajiri ya Julai 5 mwaka huu ,ambapo mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amefika Shuleni hapo kujionea hali halisi ya janga hilo.
Katika janga Hilo la Moto hakuna vifo, madhara yeyote makubwa yaliyojitokeza .
“Nichukue nafasi hii kuutarifu umma tumepata Changamoto ya tukio la Moto katika Shule yetu hii ya Chalinze Islamic Modern school ,tunamshukuru Mwenyezi Mungu hatukupata Madhara yanayohusisha athari za kifya na maisha ya wototo wetu,wakiwa katika nyumba ya ibada msikitini “Ameeleza Kunenge.
Ameeleza ,Vitu ikiwemo Sare, mabegi, sabuni, na baadhi ya madaftari walivyokuwa wakikaa navyo kwenye Bweni ndivyo vimeteketea kwa moto.
Ameeleza Shule hiyo ni kubwa wanafunzi ambao bweni lao limeungua wamepata mahali pengine pa kulala.
Hata hivyo ,Ameeleza Wataalamu tayari wameongea na vijana hao kuwatoa hofu na kuwashauri.
Kunenge amelishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani hapo kwa Elimu wanayotoa kwa Shule za Mkoa huo katika Uthibiti wa Mioto
Kunenge ametoa Rai kwa Shule zote za Mkoa huo kupata Mafunzo hayo ya Elimu jinsi ya kuthibiti madhara ya moto hatua za awali,kwenye hatua ya Ujenzi vitu gani viandaliwe, na endapo moto unatokea nini cha kufanya.
“Shule hii ilipokea Mafunzo mwezi mmoja uliopita na Moto huu ulipotokea Vijana na Jumuiya ya Wafanyakazi wa shule hii wamethibiti moto huu kutumia vizimia Moto (Mitungi) kabla gari la zimamoto halijafika” Ameeleza Kunenge.
Ameeleza ni “Fundisho zuri kwamba Elimu wameapata na Uongozi wa shule ulihakisha Uwepo wa vifaa vya Vizimia moto” amewaeleza Kunenge.
Mkuu huyo wa mkoa, ameunda timu ya kitaalamu ya kuchunguza chanzo cha moto huo ili kuchukua hatua zitakazosaidia Shule hii na Shule zingine Mkoani hapo.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani, Jenipher Shirima ameeleza kuwa moto huo ulizuka mnamo Alfajiri ya Leo 11:42, umefanikiwa kudhibitiwa mapema kupitia vizimia Moto vilivyopo shuleni hapo.
Ameeleza kutokana na Changamoto ya moto mashuleni wapo kwenye Program ya utoaji mafunzo “kila siku kuna shule ya msingi na sekondary Mkoani hapo inapatiwa mafunzo.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Chalinze Modern Islamic Primary School Bw. Omary Ismail, Ameeleza kuwa Bweni liloathirika ni la wavulana na vifaa vya wavulana 8 ndiyo vimeteketea vyote.