Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
JESHI la polisi Mkoani Pwani , linamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto wa miaka Saba ,ambae amebakwa na kuuwawa Mei 30 mwaka huu ,Misugusugu wilayani Kibaha .
Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani hapo ,Gregory Mushi alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya tukio Hilo la kinyama kisha kukimbia .
Anasema ,mkono wa sheria Ni mrefu , Jeshi Hilo limefanikiwa kumkamata ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria ,iwe fundisho kwa wengine.
Aidha ,Mushi alitaja tukio jingine lililohusisha mtoto wa kike miaka 5 mwanafunzi wa chekechea kumwagiwa mafuta ya kula ya Moto na mfanyakazi wa ndani aitwae Rehema anaekadiriwa Kuwa na miaka 14 mkazi wa Mbwewe Chalinze.
“Mtoto huyu amejeruhiwa usoni na mkono wa kulia ,,Tumemkamata baba mzazi wa mtoto baada ya kumtorosha mtuhumiwa”
Katika tukio jingine ,Mushi alieleza , jeshi la polisi kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa limemkamata mtu mmoja mwanaume (39) mkazi wa Mlandizi akiharibu miundombinu ya Tanesco na kuipatia hasara ya zaidi ya milioni 76 huko Vikuruti kata ya Mlandizi.
Alisema ,mtu huyo amekata line ya umeme ya msongo wa 33KV ambao ulikuwa unamhudumia mteja aliyetambulika kwa jina la Swai.
“Kilichotumika Ni kwamba ilichomwa Moto nguzo na kusababisha line hiyo kuanguka na kuiba waya wa alminium ACCR 100 MM2 na kulisababishia hasara ya sh.milioni 76.896.108 .
Tukio la tatu ,kusafirisha mirungi ambapo polisi walifanya msako kumkamata mtu mmoja eneo la Chalinze akisafirisha mirungi bunda 150 zenye uzito wa kg 70 kutoka Moshi mkoa wa Kilimanjaro kuelekea Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Songwe kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.254DDY Sina ya Toyota Ipsum.