NA
MWANDISHI WETU, SABASABA
WAJASIRIAMALI
wadogo na wa Kati wanayo nafasi kubwa ya kujenga maisha yao ya sasa na ya baadaye
kwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF, Meneja wa Sekta Isiyo
Rasmi wa Mfuko huo, Bi. Rehema Chuma (pichani juu), amesema.
Amesema
chini ya Mpango wa Kitaifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Isiyo Rasmi, ni muhimu
kundi hilo nalo liingie kwenye Hifadhi ya Jamii ili na wao wanapofika umri
ambao hautawawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali waweze kufaidika na
Mafao ambayo wenzao waliokuwa kwenye sekta rasmi (ajira rasmi) wanayapata.
Amewataja
Wajasiriamai hao walio katika sekta isiyo rasmi kuwa ni wote wanaofanya
shughuli za kuwapatia kipato halali na kutolea mfano, Bodaboda, Mamalishe, Machinga,
Waendesha bajaji, Mafundi cherehani, Wakaanga chipsi, Saluni za kike na kiume
na Mafundi Uashi.
“Tunaposema
tunajenga Maisha yako ya Sasa na ya Baadaye,
mwanachama atafaidika kwa kupata Mafao mbalimbali mathalan tuna Fao la Uzazi
hili litamuhusisha mwana mama ambaye alikuwa mjamzito, Fao la Msaada wa Mazishi
na Fao la Mirathi, lakini tuna Fao la Uzee ambalo hili ndio fao muhimu kwa mtu
ambaye uwezo wa kufanya kazi umekoma, mfano kwa uzee au maradhi,”alifafanua.
Meneja
huyo ambaye alikuwa akiwahamasisha wananchi wanaotembelea Maonesho ya 46 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere
maarufu Sabasaba kujiunga na Mfuko huo, Julai 2, 2022, amesema ni rahisi sana
kujiunga.
“Mwanachama
anaweza kujiunga kwenye ofisi zetu zilizoenea kote nchini na kwa wale
wanaotembelea Maonesho haya ya Sabasaba tuko banda namba 13, njoo na kitambulisho
cha NIDA au Namba, kisha utajaza fomu na kupigwa picha, na papo hapo tutakutengenezea
kitambulisho na kuwa mwanachama rasmi wa NSSF.” Alifafanua na kuongeza hata kama
mtu hana kitambulisho cha NIDA, bado anaweza kuandikishwa.
Kuhusu
viwango vya uchangiaji Meneja huyo alisema kima cha chini cha uchangianji kila
mwezi ni shilingi elfu ishirini (20,000/=) lakini anaweza kuchangia zaidi
kulingana na kipato chake.
Aidha
alisema baada ya mwanachama kupata kitambulisho chake na namba ya uanachama,
uwasilishaji michango nao pia ni rahisi,
“Sasa
hivi mfumo wa kulipa kupitia simu ndio umezoeleka sana na sisi tunatumia
utaratibu huo wa kufanya malipo ya serikali kupitia mitandao ya simu, benki au
wakala wa benki.” Alifafanua.
Aliwaondoa
hofu wajasiriamali hao kuwa hata kama kipato chake wakati mwingine
hakimuwezeshi kulipa shilingi elfu 20 kwa mkupuo, anaweza kuchangia kidogo
kidogo kama shilingi elfu 2,000/=, 5,000/= na kuendelea kupitia namba maalum ya
malipo aliyopewa (control Number) ilimradi inapotimia mwezi mwanachama awe
amekamilisha malipo ya shilingi elfu 20,000/= kwasababu Mfumo unatambua kiwango
hicho cha chini cha uchangiaji kwa mwezi.