Thobias Mwanakatwe na Dotto
Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Mhe.Elibariki Immanuel
Kingu,anatarajia kuanza ziara ambayo itadumu kwa mwezi mmoja katika kata 15 za
jimbo hilo.
Kingu katika taarifa yake leo kwa vyombo vya habari, alisema ataanza ziara
hiyo Julai 20 na kuihitimisha Augosti 20, mwaka huu ambapo katika ziara hiyo
atafanya mikutano ya hadhara na wananchi wa kata hizo.
Alizitaja kata ambazo atafanya mikutano ya hadhara kuzungumza na wananchi
kuwa ni kata ya Iyumbu, Mgungira, Mwaru, Igombwe, Irisya, Sepuka, Minyughe na
Mtunduru.
Kata nyingine ni Kituntu, Puma,Ihanja, Iseke,Iglansoni, Muhintiri na
Makilawa
Alisema mikutano hiyo ambayo itakuwa mikubwa, atatumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi mambo
yaliyopitishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2022/2023, kuwaeleza mipango ya
Serikali na kuchukua maoni ya wananchi kila kata.
“Katika mikutano hiyo ya hadhara nitawaeleza wananchi wangu mageuzi
makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu
Hassan katika nyanja zote tangu ameshika madaraka hayo,” alisema Kingu.
Aidha, alisema katika mikutano hiyo atawahamasisha wananchi kujitokeza
kujiandaa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ambalo linatarajia kufanyika Agosti
23, mwaka huu nchi nzima.
“Wananchi wote naomba tujiandae kuhudhuria kwa wingi kujua nini mwakilishi wenu amefanya katika kipindi cha
mwaka huu,” alisema.