MWENYEKITI wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe.Daniel Sillo,akisaini kitabu cha wageni mara baada kufanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga,akitoa maelezo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
MWENYEKITI wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe.Daniel Sillo,akiwa na wajumbe wake wakikagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Stanslaus Ntibara,akitoa taarifa ya ujenzi wakati wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga,akiiongoza Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
MUONEKANO wa majengo yaliyopo katika ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi.
MWENYEKITI wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe.Daniel Sillo,akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga,akiipongeza na kuishukuru Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda,akitoa taarifa kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
SEHEMU ya Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifatilia hoja mbalimbali wakati wa ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kuduma ya Bajeti Mbunge wa Viti Maalum Subira Mgalu,akitoa ushauri wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) wilayani Bahi mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Mbunge wa Ole, Juma Hamad Omary,akitoa ushauri wa ujenzi wa majengo mengine ya vyuo ikiwemo madarasa wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Bajeti katika Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) wilayani Bahi mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
Mkurugenzi wa Soko la Ajira, Mipango na Maendeleo wa VETA,Mhandisi George Sambali,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti kufanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi Mkoani Dodoma leo Julai 3,2022.
PICHA ZOTE NA ALEX SONNA
…………………………………
Na Alex Sonna-BAHI
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Bajeti imepongeza ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani Bahi ambacho kinajengwa kupitia fedha za UVIKO-19 ikiwa ni jitihada za serikali za kuimarisha eneo la ufundi.
Akizungumza katika ziara ya kamati hiyo leo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Daniel Sillo, alisema Mkuu wa Wilaya ya Bahi pamoja na timu yake wamefanya kazi nzuri ya usimamizi na kuwataka waendelee kusimamia miradi ya serikali.
“Sisi kamati tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono makubwa aliyonayo juu ya taifa letu ikiwa ni pamoja na fedha zilizoelekezwa kwenye maeneo haya mahsusi hasa kubwa likiwa hili la ufundi, tunatarajia baada ya kukamilika vijana wetu watasoma na kupata ufundi na kujiajiri,”amesema.
Amesema kamati hiyo ilipewa jukumu kwa niaba ya Bunge la kupanga matumizi ya fedha za UVIKO-19 ambazo Tanzania ilipata mkopo kutoka IMF na kwamba wanajivunia fedha hizo kuelekezwa kwenye maeneo muhimu ikiwamo ujenzi wa vyuo vya VETA.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga, amesema Sh.Bilioni 20 kati ya Sh.Bilioni 64.9 zilizotolewa kwenye mgawanyo wa fedha za UVIKO-19, zilitengwa kwa ajili ya umaliziaji wa vyuo vya VETA 25.
“Sh.Bilioni 8.7 zilikuwa kwa ajili ya samani ambazo unaziona sasa na hata kule Kilindi tayari zimeshakwenda, lakini Sh. Bilioni 20 nyingine tuliipeleka kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyuo vya Mikoa katika Mikoa minne ambapo ipo Njombe, Rukwa, Simiyu na Geita,”amesema.
Amebainisha kuwa Sh.Bilioni moja imepelekwa Chuo cha Morogoro cha Ualimu kwa ajili ya walimu wa vyuo vya ufundi.
“Kulikuwa na bweni moja ambalo lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 lilikuwa bado halijaisha tukasema tulimalize ili kuongeza udahili wa masuala ya ufundi, na Sh.Bilioni 6.8 zimepekekwa kwa ajili ya Vyuo vyetu vya FDC, ambapo tuna FDC 54 Tanzania nzima na kulikuwa hakuna vifaa tukasema tupeleke vifaa vya kujifunzia na kufundishia,”amesema.
Kipanga amesema fedha nyingine imepelekwa kwa watu wenye ulemavu kwa kununua vifaa mbalimbali ikiwamo vya kujifunzia.
Kuhusu chuo hicho cha Bahi, amesema zilipelekwa Sh.Milioni 695 ambazo hazitoshi kugharamia kazi za nje , kuingiza umeme, maji na kutengeneza barabara za kuingia chuoni hapo.
“Chuo tunatarajia kikamilike Mwezi wa Oktoba hadi Novemba mwaka huu ili kianze kudahili na ifikapo Januari mwakani vyuo vyote 25 vianze kutoa elimu ya ufundi kutokana na kuwapo kwa mahitaji makubwa ya elimu hiyo,”amesema.
Naye Mbunge wa Viti Maalum,ameshauri kupitiwa upya kwa mitaala ya vyuo vya VETA hususani ijielekeze katika nchi kufunguka ili iendane na kozi ambazo watazitoa kwenye chuo hicho.
“Utalii ulivyofunguka tuangalie masuala mazima ya hospitality (huduma) namna ya kusaidia mahoteli makubwa yaliyofunguliwa. Badala ya utaratibu wa zamani wa kutoa wafanyakazi katika nchi za jirani tujielekeze katika vyuo vya kati ili kuleta ushindani katika uchumi uliofunguka,”amesema.
Awali, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi George Sambali amesema chuo kitakapokamilika kitatoa kozi za muda mfupi kwa miezi sita hadi 12 ambazo ni pamoja na udereva na ushonaji.