Na Mwamvua Mwinyi
Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Ridhiwani Kikwete amewaasa maafisa ardhi kutimiza wajibu katika utendaji wao kazi .
Aliwaambia ,kila mmoja afanye kazi kikamilifu ili kupunguza ama kuondoa changamoto zinazohusiana na masuala ya ardhi ndani ya jamii.
“Baada ya ufungaji wa Mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi yaliyofanyika Chuo Cha Mkwawa, Iringa nilipata nafasi kuzungumza na Maafisa Ardhi wa Mkoa wa Iringa na Manispaa ya Iringa.”alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alibainisha kwamba, Lengo ni kujadili hali ya Kazi na kukumbushana Wajibu wa kila mmoja katika Utendaji.
#KaziInaendelea #ArdhiYetuIringa