************************
JIJI la Hamburg nchini Ujerumani na Dar es Salaam wamesaini mkataba wa mashirikiano katika maeneo matano ikiwemo sekta ya elimu, afya, ujasiriamali na sanaa.
Mkataba huo ulisainiwa leo Jijini Dar es Salaam kati ya Meya wa hili, Omary Kumbilamoto na mwenzake wa Hamburg nchini Ujerumani.
Akizungumza muda mfupi baada ya kusaini makubaliano hayo, Kumbilamoto amesema mkataba huo pia una lengo kupendezesha jiji la Dar es Salaam na kwamba itasaidia kutangaza Tanzania kimataifa na kukuza uchumi.
“Niwapongeze wenyetu wa jiji la Hamburg kwa upendo wao kwenye na kujitoa kusaidia katika sekta mbalimbali hasa ya mazingira baada ya kuhaidi kutupatia fedha za kupendezesha mji wetu,” anesema Kumbilamoto.
Amesema ujuo wa ugeni huo ni matokeo ya kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuitangaza Royal Tour kimataifa na kuisaidia nchi kupata manufaa.
Aidha Kumbilamoto amesema mashirikiano hayo yaliyopo baina ya miji hiyo miwili yanatakiwa kudumishwa na kuendelezwa kwa sababu yanaleta umoja katika taifa.
Amesema kama viongozi wanaendelea kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza nchi kimataifa pia kujenga uchumi.
“Tunapowakaribisha wageni kuja nchini watakuja na fedha watazitumia katika mambo mbalimbali hiyo itatusaidia kuongeza mapato ya ndani na wafanyabiashara kufanya biashara na kujiongezea kipato,”amesema na kuongeza
“Haya ndo matendo ya Royal Tour imefanya wageni kuja na faids kubwa ni kupata mapato ya ndani kutokana na utalii,pato linakuja linaongezeka na linasaidia kutatua changamoto za wananchi, “amesema Meya Kumbilamoto
Kwa Upande wake Ofisa Mkazi Mji wa Hamburg jijini Dar es Salaam, Jinken Bruns amesema wataendeleza mashirikiano na jiji la Dar es Salaam katika mambo mbalimbali.
Amesema ushirikiano huo waliosaini jana utalenga katika sekta mbalimbali ambapo itasaidia kukuza uchumi na kuongeza mapato.
“Tunaadhimisha miaka 12 ya ushirikiano wetu baina ya Jiji la Dar es Salaam na Hamburg na urafiki huu utaendelea kuimarika siku zote katika kusaidiana mambo mbalimbali,”anesema
Naye Mwenyekiti wa wadau wa ushirikiano mji wa Dar es Salaam, Michael Onesmo amesema mahusiano hayo yatakwenda kuinua mapato ya jiji na kuongeza ajira hasa kwa vijana.
“Moja ya manufaa ya mahusiano haya kati ya jiji la Dar es Salaam na Hambury yatakwenda kuboresha uchuni wetu kwa kuongeza mapato ya jiji na kuongeza cha ajira,” amesema