************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAKALA wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti ya kupanda na asili la Sao Hill Mkoani Iringa wilaya ya Mufindi wamesema majanga ya moto yamepungua kutokana na elimu ambayo wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara juu ya madhara yanayotokana moto.
Akizungumza wakati wa usahili wa vijana wa kupambana na moto Mhifadhi mkuu Msaidizi Tarafa ya nne Mgololo,Lukiko Maiila Alisema kuwa wamekuwa wanaajili mara kwa mara wafanyakazi kwa ajili ya kupambana na moto katika tarafa hiyo.
Maiila Alisema kuwa wamekuwa wanasaidia kuzima na kupambana na moto kipindi ambacho kunakuwa kimetokea kwa majanga hayo.
Alisema kuwa moto umekuwa unaleta madhara ya kiuchumi kwa shamba la Sao Hill na wananchi ambao wamekuwa wanalima mazao ya misitu.
Maiila alisema kuwa wamekuwa wanatoa elimu mara kwa mara juu ya madhara ya moto kwa wananchi wote wanaolizunguka shamba la miti la Sao Hill.
Alisema kuwa wamefanya usahili wa vijana mia moja thelethini na saba (137) kutoka Vijiji kumi na mbili (12) na wanaotakiwa kuajiliwa ni vijana 49 katika Kijiji cha Kitasengwa kata ya Makungu.
Maiila alisema kuwa wamefanya usahili wa ukakamavu kwasababu maeneo ambayo wanaenda kufanyia kazi yanamiinuko mingi hivyo walipokuwa na utimamu wa mwili hataifanya kazi inavyotakiwa
Alisema kuwa tarafa ya nne ya shamba la Sao Hill wanatarajia kuajili wafanyakazi 2000 ambao watakuwa wanafanya kazi mbalimbali katika tarafa hiyo kwa lengo la kulinda na kuitunza miti ambayo ipo katika shamba la Sao Hill.
Maiila alimazia kwa kusema kuwa hawatarajii kupata majanga ya moto katika kipindi hiki cha kiangazi ambacho mara nyingi majanga hayo ndio hujitokeza.
Kwa upande wake baadhi ya wananchi wanaolizunguka shamba hilo wamesema kuwa limesaidia kutoa elimu ya madhara ya moto na kupunguza majanga ya moto kutokea mara kwa mara.
Walisema kuwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara imesaidia wananchi wengi kuwa na uelewa mpana wa namna gani ya kuzuia kusitokee janga la moto.