Na Silvia Mchuruza,Bukoba, Kagera.
Ni katika muendelezo wa maonesho ya kibiashara ya Africa mashariki yanayofanyika mjini Bukoba ambapo nchi zilizoshiliki mpaka Sasa katika maonesho hayo ni Uganda,Rwanda,Burundi,DRC Congo pamoja na wafanyabiashara kutoka katika mikoa mbalimbali nchi.
Akizungumza katika maonesho hayo afisa habari wa kiwanda Cha utengenezaji wa wine kinachojulikana kwa jina la KOMBUCHA WINE mkoani kagera katika halmashauri ya wilaya ya Karagwe katika mji wa kayanga ndg. Yese Kagenzi amesema kuwa uwepo wa maonesho hayo ya Africa mashariki ni mwanzo wa kukuza kipato Cha wafanyabiashara na mkoa kwa ujumla.
Amesema kiwanda hicho mpaka sasa nimekuwa kikiongeza thamani ya mazao ya kiasili ya mkoa kwa utengenezaji wa wine hiyo unatumia mimea ya asili Kama vile kashwagara, mkalitusi,tangawizi, zabibu na mchaichai na kuongeza kuwa ndiyo wazalishaji wa kwanza wa kinywaji Aina ya wine
“Tunatumia mimea ya asili kukuza thamani ya bidhaa zetu na Ni mimea tuliyonayo katika mazingira yetu na pia tunaitafuta kwa wananchi tunawaingizia kipato kwa kununua vifaa vya utengenezaji wa wine yetu pia mpaka sasa tunatoa ajira kwa vijana pia zaidi ya vijana 30 wameajiliwa tayali.” alisema Ndg.Yese.
Vinywaji vyetu mpaka Sasa tumezifikia nchi jirani na pia katika mikoa mbalimbali tumefika kwa kuendelea kuifikishia jamii ya kitanzania juu ya kazi tunazo zifanya.
Pia nao baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchi za Uganda na Rwanda akiwemo Ndg.Minan Frolibat kutoka cooperative ya omurumuli bujumbura Burundi ameshukuru kufunguliwa kwa mipaka ya Tanzania kwani kupitia maonesho hayo wamejivunia vitu vingi Kama kushirikiana kiubunifu.
Licha ya hayo ametoa wito kwa vijana wa kitanzania kujiajili kupitia kazi za mikono na kupitia Ubunifu ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi.