Waandishi na baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri ya jiji wakufuatilia kwa makini mkutano huo wa wanahabari ambao umefanyika jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Dkt Sylvia Ruambo akizungumza mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani. Kuhusu mapokezi ya wageni kutoka Hamburg. wengine nisehehemu ya wanakamati.
******************
Mwandishi Wetu
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam linatarajia kupokea ugeni wa watu zaidi ya 30 kutoka katika Jiji la Hamburg Nchini Ujerumani kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 12 ya urafiki wa miji hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo juni 28, 2022 Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Dkt. Sylvia Ruambo amesemakuwa wageni hao wataingia juni 30 mwaka huu ambapo wakiwa hapa nchiniwatajadili changamoto na fursa zinazotokana na mabadiliko ya tabianchikwa manufaa ya wananchi wa majiji hayo.
Amesema kuwa wadau watakaoshiriki wanatoka katika taasisi mbalimbali za serikali ,Asasi za kirai na sekta binafsi ambapo kwa kupitia fursa hiyo wameona kuna umuhimu wa kukutana na kufanya majadiliano ikiwa nisehemu ya juhudi za kushirikiana na serikali katika jitihada za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
”Urafiki kati ya majiji haya umechangia na kusaidia kuboresha huduma katika sekta mbalimbali hususani jiji la Dar es Salaam ikiwamo sekta Afya ,mazingira,utafiti ,elimu.na utamaduni . pia majiji haya yamesaidia watalaamu wake na wananchi kufanya ziara za kujifunza
kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi na utekelelzaji wa miradi.”Amesema
kwaupande wake mjumbe kamati kuu Francisca Damian amesema katika kipindi cha miaka 12 ya urafiki huo Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ,chuo kikuu cha Ardhi,na jiji la Hamburg wamekuwa na mstari wa
mbele katika uandaaji wa mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,kufanya tafiti kuhusu athari zinazoweza kusababishwa mabadiliko ya tabianchi na namna ya kukabiliana nazo.
Amefafanua urafiki wa jiji la Dar es Salaam na Hamburg uliaza baada ya kutiliana saini ya hati ya makubaliano hivyo maadhisho hayo ya 12 yanatarajia kuwakutanisha wadau mbalimbali ambao watashauliana njia
bora ya kuimarisha urafiki huo na kuongeza idadi ya watu watakaonufaika na fursa zitokanazo na mahusiano yaliyopo.