Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wataalamu wa Uthamini Juni 30, 2022 kinachoendelea jijini Dodoma. Kulia ni Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha na kushoto ni Msajili wa Bodi ya Uthamini Joseph Shewiyo.
Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha akizungumza wakati wa kikao kazi cha wataalamu wa Wathamini kinachoendelea jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi na kushoto ni Msajili wa Bodi ya Uthamini Joseph Shewiyo.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha wataalamu wa Uthamini kinachofanyika mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi (Wa tatu kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa uthamini wanaoshiriki kikao kazi jijini Dodoma. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi amewataka wataalamu wa utahamini kujitathmini katika kazi wanazozifanya ili kuepuka kufanya kazi kwa matakwa ya wale wanaowafanyia kazi.
Alisema zipo tafiti mbalimbali zilizofanyika zikionesha asilimia kubwa ya kazi zinazofanywa na wataalamu wa uthamini zina ushawishi wa watu wanaozihitaji jambo alilolieleza kuwa halileti picha nzuri.
‘’Tafiti zinaonesha kazi nyingi mnazozifanya asilimia kubwa zinakuwa ‘influenced’ na matakwa ya wale wanazohitaji hiyo haileti picha nzuri kama watendaji wa serikali na wale walioaminiwa kukabidhiwa kazi’’. Alisema Dkt Kijazi
Akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili cha wataalamu wa uthamini kinachoendelea jijini Dodoma tarehe 30 Juni 2022, Dkt Kijazi aliwaambia wataalamu hao kuwa, wakati wakiendelea na kikao chao ni vyema wakajitathmini na kujiuliza ni nini kifanyike kuzuia hali hiyo isiendeleeea kwa kuwa inasabisha utaaluma usioziungatia maadili na kuleta matokeo ya ufanyaji kazi kwa kuzingatia matakwa ya wanaofanyiwa kazi badala ya kuzingatia sheria na miongozo.
‘’Kuna umuhimu wa kujipanga na kufanya mabadiliko katika utendaji kazi ili kuepuka mfumo wa kufanya kazi lkwa mazoeza na kuwa na mifumo iliyojengwa ikiwa imara na itakayoisaidia wizara kutoa huduma zilizo bora zaidi’’. Alisema Dkt Kijazi
Kwa upande wake Mthamni Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha alisema katika juhudi za ofisi yake kuepukana na changamoto za uthamini wamejipanga kutoa elimu na kuwa wawazi wakati wote wa kufanya kazi zake.
‘’Sasa hivi kwenye mikakati yetu tumejipanga Kutoa elimu sambamba na kuwa wawawezi wakati wa utendaji wetu wa kazi, zamani wakati wa kufanya uthamini mtu hajui atapata kiasi gani lakini kwa sasa ni tofauti kabla ya fidia mwananchi anaoneshwa jedwali la uthamini na kuelezwa kama ana miembe mingapi au nyumba ngapi ndiyo asaini asipokubaliana hatuendelei na kazi’’. Alisema Evelyne
Kwa mujibu wa Mthamini Mkuu wa Serikali, utaratibu huo umesaidia sana kuondoa changamoto kwenye uthamini na kutolea mfano wa uthamini wa mradi wa reli ya SGR kutka Dar es Salaam ambao unakaribia mkoani Mwanza kuwa, hakuna mgogoro wowote uliojitokesa kutoka na uwazi na elimu kwa wananchi.
Kikao hicho cha siku mbili cha wataalamu wa uthamini kinashirikisha wataalam kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na kinajadli mambo mbalimbali kama vile uidhinishaji taarifa za uthamini, uhuishaji jedwali la viwango vya mazao, utekelezaji mazoezi mbalimbali ya uthamini wa fidia ikiwemo ule wa miradi ya kimkakati.