NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga, akizungumza na wazazi wa shule za msingi za kata ya Ipagala kwenye hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza na wazazi wa shule za msingi za kata ya Ipagala kwenye hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
Naibu wazairi wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma mjini Antony Mavunde,akizungumza na wazazi wa shule za msingi za kata ya Ipagala kwenye hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,akizungumza na wazazi wa shule za msingi za kata ya Ipagala kwenye hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
SEHEMU ya Walimu,Wananfunzi na Wazazi wakifatilia hotuba mbalimbal wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana wazazi wa shule za msingi za kata ya Ipagala.
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Omary Kipanga, akiwakabidhi vyeti na zawadi mbalimbali walimu na wanafunzi waliofanya vizuri wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana kwa shule za msingi za kata ya Ipagala kwenye
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi mara baada ya kumaliza kwa hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana kwa
shule za msingi za kata ya Ipagala kwenye
…………………………………………..
Na Eva Godwin-DODOMA
NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga,amewapongeza Walimu wa Shule ya Msingi Mtemi Mazengo kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
Kipanga ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wazazi wa shule za msingi za kata ya Ipagala kwenye hafla ya kuwapongeza walimu kwa kuwezesha idadi kubwa ya wanafunzi kufaulu katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
“Kwanza tuwapongeze Walimu kwa kuwalea na kuwafundisha Wanafunzi wetu nidhamu maana inaonyesha nidhamu yao ipo juu na ndio maana ufaulu wao pia upo juu “Tulitegemea labda huenda shule za International ndio zingeongoza,lakini tumefurahi zaidi kuona Shule za Msingi pia zinafanya vizuri”,amesema
” Katika Bajeti hii tuliyoimaliza juzi Rais Samia Suluhu ametuagiza kutenge fedha bilioni 40 kwalajili ya kujenga Chuo kikubwa cha Tehama hapa Jijini Dodoma Nara, hiki kitakuwa chuo cha mfano”.amesema Kipanga
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka, amewataka Walimu wajenge ushindani wa kuwa na ufaulu wa kitaifa kutoka Shule za Serikali,Kuanzia Sekondari na Msingi.
“Matokeo mazuri ni ushindani lakini pia Matokeo mazuri ni Mzazi,Mtoto na Mwalimu, Walimu wanapaswa kueshimiwa na kutunzwa” ,amesema
“Na ufaulu wa Mtoto ndio utakaompeleka Shule najua mnalitambua hili na muendelee kulitambua hili kwa Wazazi wote lakini”.amesema Mtaka
Aidha Mtaka amesema kuwa katika kipindi atakachokuwa mkoani hapa ajenda yake kubwa ni elimu ili kuutoa mkoa wa katika nafasi za mwisho kitaifa.
“Katika matokeo ya mwaka unaokuja zile nafasi za Dodoma kuwa mkia hapana hatutaruhusu tena na hivi sasa tupo katika mchakato wa kununua mashine kubwa ya kuprinti mitihani print unit ya mkoa ambayo itakuwa na uwezo wa kuchapisha mitihani ya mkoa mzima ili watoto wetu wapate mazoezi ya kutosha”amesema
Naye Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri, amewataka Wazazi kuwa na ukaribu na Watoto wao pamoja na kuwashauri wawe na Marafiki wenye shauku ya Ufaulu ili kuepuka tabia zisizo faa kwa Watoto.
“Wazazi ongeeni na watoto wenu kuchagua marafiki wenye tabia bora kumeibuka kwa tabia za urawiti kwa watoto mashuleni ongeni na watoto wenu ili kudhibiti tabia hizo watoto wanafanyiwa lakini wakaa kimya hivyo ni wajibu wenu kuchukua hatua”amesema Shekimweri
Kwa upande wake Naibu wazairi wa Kilimo na Mbunge wa Dodoma mjini Antony Mavunde, amewataka wazazi kuwapa ushirikiano walimu ili kuwasaidia watoto kufanya vizuri katika masomo yao.
“Wazazi tuwape ushirikiano waalimu wetu kwani wao ndiyo wanakuwa na watoto wetu kwa muda mrefu tunataka Dodoma kufanya mapinduzi katika sekta ya elimu lazima tuutangaze mkoa wetu kwa ufaulu mzuri hatutaki kuwa Dodoma ile ambayo mtu akiwa na shida ya msichana wa kazi simu ya kwanza anapiga Dodoma na Iringa utamaduni huo lazima ufe mara moja”amesema Mavunde