Mkurugenzi mtendaji wa Hakielimu Dk.John Kalage akizungumza katika uzinduzi uzinduzi huo jijini Arusha leo
Kamishna wa ustawi wa jamii Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalumu ,Dk Nandera Mhando akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha
Kamishna wa ustawi wa jamii Wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalumu ,Dk Nandera Mhando akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha
………………………………….
Julieth Laizer ,Arusha.
Kamishna wa ustawi wa jamii wa wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na makundi maalumu,Dk Nadera Muhando amezindua miongozo kitaifa wa uundaji na uendeshaji wa mabaraza ya watoto Tanzania pamoja na madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto ndani na nje ya shule.
Akizungumza Leo jijini Arusha kwenye mkutano mkuu wa sita wa wadau wa elimu kutoka nchi tatu za jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa uzinduzi huo ,Dk Muhando amesema kuwa, miongozo hiyo imezinduliwa kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatii katika maeneo mbalimbali nchini.
Dk Muhando amesema kuwa,miongozo hiyo ni moja ya mikakati ya kusaidia kupunguza ukatili kwa watoto ambapo inalenga kuwafikia watoto na wanawake kwani Kwa pamoja tumepewa jukumu kubwa la kumlinda mtoto chini ya sheria namba 21 ya 2009 pamoja na marekebisho madogo ya mwaka huo ambapo ni wajibu wetu kumlinda mtoto katika makao mbalimbali,nyumba salama na walioko mitaani.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa haki elimu ,Dk.John Kalage amesema mkutano huo umewakutanisha mashirika 13 kutoka Uganda,Kenya na Tanzania ambao ni mahususi kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali pamoja na ubadilishanaji wa uzoefu wa masuala ya kuzuia na ukatili kwa watoto ambao unafanyika nje na ndani ya shule.
“Tumeamua kubadilisha uzoefu ili shule ziwe salama kwa watoto kujifunza pamoja na kuwaondolea hofu pindi wanapoenda na kurudi shuleni kwani pamoja na uwepo wa sheria mbalimbali bado vitendo hivyi vimekithiri katika baadhi ya maeneo mbalimbali,”amesema Dk.Kalage.
Dk.Kalage amewataka wananchi kuendelea kufichua na kutaoa taarifa katika vyombo husika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake dhidi ya mtuhumiwa na vitendo vya ukatili viweze kupungua na watoto waweze kuwa salama na kujifunza ipasavyo.
Naye Afisa ustawi wa jamii wa mkoa wa Arusha,Denis Mgiye amesema kuwa,anashukuru wadau kwa kushirikiana na serikali kuzindua miongozo hiyo iliyolenga katika kuhakikisha watoto wanalindwa lakini bado wanaendelea kupambana na masuala ya ukatili.
“Srikali kwa kushirikiana na wadau wanafanya juhudi katika kukabiliana na vitendo hivyo lakini changamoto ni baadhi ya familia kumalizia kesi nyumbani hali ambayo inachangia kuongezeka kwa matukio hayo,”amesema.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo,Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya Arusha,Angela Mvaa amesema wamekuwa wamekuwa wakitoa elimu ya vitendo vya ukatili kwa kushirikiana na jamii ili kuweza kuweza kuvitokomeza.