**************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,alhaj Abubakar Kunenge ametoa Rai kwa Maafisa Biashara wa Mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Lindi na Mtwara kuhakikisha Jitihada za Serikali awamu ya sita za Kuvutia Wawekezaji zinafikiwa,ikiwa Ni Pamoja na kuchangamka Kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo vipya .
” Rais Samia Suluhu anavutia Wawekezaji na ameshasema nini kifanyike jinsi gani hayo yanatekelezeka Maafisa Biashara mnapaswa kufanya, Vinara wa Utekelezaji ni ninyi Maafisa Biashara tuone Uwepo wenu (Visibility). Lazima muelewe matarajio ya Nchi ili muyatimize.
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea Uwezo Maafisa Biashara wa Mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Mtwara na Lindi.
Amewaeleza kuwa Serikali imeamua kuanzisha Idara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuongeza ufanisi wa Sekta hiyo.
Amewataka kuhakikisha wanatoa huduma Bora kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara.
“Lazima tutoe huduma bora, lazima tujue wateja wetu ni Wafanyabiashara, huduma bora inabadilika mara kwa mara kwa Wafanyabiashara” Ameeleza Kunenge.
Amewaeleza kuwa Tanzania tupo eneo la Kimkakati Strategic position na kila Afisa Biashara anatakiwa kujua Fursa za Uwekezaji zilizopo kwenye Eneo lake.
Amewataka kusoma na kutumia Takwimu za Taasisi mbalimbali katika Kushauri na Kufanya Maamuzi “Wawekezaji wanapokuja manawapa Takwimu gani? Amehoji Kunenge-
“Wajibu wenu kuhakikisha Spidi ya Teknolojia mnakwenda nayo mkishindwa mtakuwa hamfai Maafisa Biashara mnatakiwa msome kila kitu” amesitiza Kunenge
Ameeleza kuwa utafiti unaonesha Maafisa Biashara wanatumika zaidi kama wakusanya Mapato badala ya kuwa wasaidizi na washauri wa Wafanyabiashara na Wawekezaji.
Amewataka baada ya mafunzo hayo kubadilisha fikra na mitazamo yao na kuwa watoa huduma na msaada kwa Wafanyabiashara.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa Amewataka Maafisa Biashara hao kutokuwa maafisa Biashara wa Ofisini badala yake kuwasadia na Kushauri Wafanyabiashara.
Hata hivyo ,amekemea tabia ya baadhi ya Maafisa Biashara kufoji Leseni za Biashara Daraja B na kuwaeleza kuwa sasa wameandaa mfumo ambapo leseni zote zitatolewa kwa njia ya mtandao.