zaidi ya hekari 110 uliokuwepo baina ya wawekezaji na wananchi wa Kijiji cha
Ufyambe.
Mmoja ya wawekezaji akiongea na wananchi wakati wa kutatua mgogoro wa ardhi wa
zaidi ya hekari 110 uliokuwepo baina ya wawekezaji na wananchi wa Kijiji cha
Ufyambe.Wawekezaji wakiongea na wananchi wakati wa kutatua mgogoro wa ardhi wa zaidi ya hekari 110 uliokuwepo baina ya wawekezaji na wananchi wa Kijiji cha Ufyambe.Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wakati wa kutatua mgogoro wa ardhi wa zaidi ya hekari 110 uliokuwepo baina ya wawekezaji na wananchi wa Kijiji cha Ufyambe.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi wa
zaidi ya hekari 110 uliokuwepo baina ya wawekezaji na wananchi wa Kijiji cha
Ufyambe.
Akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara,mkuu wa wilaya Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa alipokea malalamiko ya
wananchi juu ya wawekezaji hao kuwa wamechukua eneo la ardhi bila ridhaa ya
wananchi.
Moyo alisema kuwa kazi ya serikali ya
wilaya ni kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto za wananchi pamoja na
kuwasimamia katika maendeleo hivyo jukumu alilofanya alitimiza kama ambavyo
inatakiwa iwe.
Alisema kuwa kitendo cha kuwaweka
ndani viongozi wa serikali ya kijiji cha Ufyambe kilikuwa kitendo cha kutaka
kupata ushahidi wa nini kinaendelea kwenye mgogoro wa ardhi baina ya wananchi
na wawekezaji.
Moyo alisema kuwa serikali lazima
inafanye kazi kwa mjibu wa katiba na sheria za nchi katika kuwatumikia wananchi
ndio maana wamefanikiwa kutatua mgogoro huo.
Alisema kuwa wawekezaji walikiuka
baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yanaenda kinyume na kanuni za uwekezaji wa
ardhi ya Kijiji hivyo baada ya kubaini hilo wawekezaji walifuata sheria zote.
Moyo aliwataka wawekezaji wote ambao
wapo na wanataka kuwekeza katika ardhi ya wilaya ya Iringa wanatakiwa kufuata
taratibu na sheria za uwekezaji ili wasibuguziwe.
Alisema kuwa wananchi wanapaswa
kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji waliopo katika maeneo mbalimbali
wanayazunguka ili kupata faida ya uwepo wa wawekezaji kama ambavyo wawekezaji
wamekuwa wakichangia maendeleo kwenye miradi mbalimbali ya ujirani mwema.
Aidha Moyo alisema kuwa serikali ya
awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anawakaribisha wawekezaji na anawapenda
wawekezaji lakini anataka wawekezaji wafuate taratibu, sheria,kanuni na Katiba
ya nchi.
John Lemomo,Baton Nsemwa na mchungaji
Metili walisema kuwa walifanya kosa walipofika kuwekeza katika hatua za awali
na kupeleka mgogoro ambao umetatuliwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed
Hassan Moyo.
Walisema kuwa wanamshukuru mkuu wa
wilaya ya Iringa kwa kuwakumbusha kufuata taratibu na sheria za uwekezaji ili
kuepukana na migogoro baina yao na wananchi wa maeneo husika.
Waliongeza kuwa wapo tayari kuwekeza
katika Kijiji cha Ufyambe na wataendelea kutoa elimu kwa wawekezaji wengine
ambao wanania ya kuwekeza ili wafuate taratibu na sheria za uwekezaji
zinavyotaka.
Nao baadhi ya wananchi walisema kuwa
wanakaribisha tena wawekezaji hao na wafanye uwekezaji wao kwa kufuata taratibu
na sheria za uwekezaji ili kuepukana na migogoro baina ya wananchi wa Kijiji
cha Ufyambe.