Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu akikabidhi vyeti na zawadi kwa washindi wa fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye pamoja na baadhi ya viongozi wa Chuo hicho wakipata picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Fainali za shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu akizungumza katika fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza katika fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Utafiti, Prof.Bernadeta Killian akizungumza katika fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo. Baadhi ya wadau wa Ubinufu na ujasiliamali wakifuatilia fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo. Baadhi ya wabunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakitoa burudani ya ngoma fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu (mwenye kaunda suti) akiwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye (mwenye tai ya blue) wakitazama baadhi ya bunifu uliofanywa na wanafunzi wabunifu wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam katika fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam lililofanyika leo Juni 25,2022 Chuoni hapo.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************
NA EEMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Vijana hususani wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wametakiwa kuacha ubinafsi katika kutafuta fursa za uwekezaji zinazotokana na ujasiliamali na ubunifu wanaozalisha wakiwa katika masomo yao.
Ushauri huo umetolewa mapema leo Juni 25,2022 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt Amos Nungu katika fainali za Shindano la Mwaka la Ubunifu na Ujasiliamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Akizungumza katika hafla hiyo Dkt.Nungu amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya kila alichodai umimi ambapo akitokea muwezeshaji akaahidi fedha na kuhitaji asilimia kadhaa vijana wengi hukataa jambo ambalo huwarudisha nyuma vijana wengi katika kuanzisha miradi mbalimbali.
Aidha amewataka vijana kujenga desturi za kushirikiana na kutengeneza mtandao wa watu mbalimbali katika masuala ya ubunifu na ujasiliamali ili kuweza kupata manufaa zaidi ya kufanikiwa katika ndoto zao za kuonekana, kusikilizwa na kuendelezwa.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye amesema Chuo hicho kipo katika mchakato wa kuanzisha kituo kikubwa zaidi cha Ubunifu na Ujasiriamali (Innovation Hub) kwaajili ya kupanua na kuimarisha shughuli za ubunifu na ujasiriamali.
“Kituo hiki kitapanua nafasi ya kuatamia kampuni changa (Startup na Spinoff companies) ambazo zitatokana na wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo, lakini pia kutoka kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati”. Amesema Prof.Anangisye.
Amesema kituo hicho kitapanua wigo wa kushirikiana na viwanda na wafanyabiashara ambao watapenda kulea na kufadhili bunifu mbalimbali ambazo zinatokana na kazi za tafiti za Chuo Kikuu.
“Makampuni hayo yanaweza kuingia mikataba kuingia mikataba na Chuo ya kuchukua matokeo ya bunifu hizo pale zitakapokamilika”. Amesema
Nae Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Utafiti, Prof.Bernadeta Killian amesema katika mwaka huu yamekuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi ambapo kulikuwa na makundi yapatayo 188 ya wananfunzi 627 ambao walijiunga kutengeneza mawazo ya ubunifu na ujasiriamali ambayo yanalenga kutatua changamoto za kijamii.
Aidha amesema maandiko hayo yalichujwa hadi kubaki 20 tu. Wamiliki wa mawazo hayo 20 ya ubunifu na ujasiriamali walipata nafasi ya kushindanisha mawazo yao mbele ya jopo la wataalamu katika nusu fainali iliyofanyika Mei 28,2022.
“Mawasilisho hayo yalichujwa hadi kubaki 7, na zaidi ya hapo Juni 4,2022 wamiliki wa mawazo hayo 7 walipewa fursa ya kujengewa uwezo kupitia mafunzo ya jinsi ya kuwasilisha wazo la biashara na elimu ya awali kuhusu miliki bunifu”. Amesema Prof.Killian.
Ameeleza kuwa timu hizo 7 ambazo zimeshindanishwa leo kupata washindi watatu ambapo wamezawadiwa Shilingi Milioni 10 kwa mshindi wa kwanza,Milioni 7.5 mshindi wa pili na Milioni 5 kwa mshidi wa tatu.
Amesema washindi watatakiwa kuleta mpango kazi wa matumizi ya fedha hizo kwa lengo la utekelezaji wa mawazo yao.