Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka akizungumza wakati wa zoezi la kupokea mashine ya kudurufu nyaraka (photocopy mashine) kutoka kwa taasisi ya huduma ya Umega iliyochini ya Nabii Samweli Rolinga iliyotolewa kwa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu, tukio lililofanyika katika shule ya Dodoma sekonadri.
Nabii Samweli Rolinga akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi mashine ya kudurufu nyaraka (photocopy mashine) waliyoitoa kwa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu tukio lililofanyika katika shule ya Dodoma sekonadri.
Afisa elimu wa Mkoa wa Dodoma mwalimu Gift Kyando akizungumza wakati wa zoezi la kupokea mashine ya kudurufu nyaraka (photocopy mashine) kutoka kwa taasisi ya huduma ya Umega iliyochini ya Nabii Samweli Rolinga iliyotolewa kwa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu tukio lililofanyika katika shule ya Dodoma sekonadri.
Mkuu wa shule ya Dodoma sekondari Mwalimu Francis Kyando akizungumza wakati akipokea mashine ya kudurufu nyaraka (photocopy mashine) kutoka kwa taasisi ya huduma ya Umega iliyochini ya Nabii Samweli Rolinga iliyotolewa kwa Shule hiyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu tukio lililofanyika katika shule ya Dodoma sekonadri.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka wa kwanza kushoto akipokea mashine ya kudurufu nyaraka (photocopy mashine) kutoka kwa Nabii Samweli Rolinga iliyotolewa kwa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika elimutukio lililofanyika katika shule ya Dodoma sekonadri.
Nabii Samweli Rolinga wa tano kutoka kushoto waliosimama mstari wa kwanza akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi viongozi wa vyama vya kidini katika shule ya sekondari Dodoma na viongozi wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya tukio la kukabidhi mashine ya kudurufu nyaraka (photocopy mashine) waliyoitoa kwa Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu tukio lililofanyika katika shule ya Dodoma sekonadri.
…………………………………………
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amezihimiza taasisi za kidini kuacha kuendekeza migogoro katika taasisi zao na badala yake wajikite katika kuhimiza maadili na kutatua changamoto zinazowakabili wanajamii katika maeneo yao.
Mtaka ametoa wito huo jijini Dodoma wakati akipokea mashine ya kudurufu nyaraka (photocopy mashine) kutoka kwa taasisi ya huduma ya Umega iliyochini ya Nabii Samweli Rolinga iliyotolewa katika Shule ya Sekondari Dodoma.
Ambapo amesema taasisi za kidini zinawajibu wa kuhakikisha zinawakumbuka wanajamii kwa kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili katika maeneo yao hasa suala la elimu kwani bado linachangamoto nyingi kwa baadhi jamii kushindwa kupeleka watoto wao shule kwa kukosa vitu vidogo vidogo.
“Inabidi mnapokemea mapepo pia mkumbuke bado jamii zetu katika maeneo mbalimbali bado wanachangamoto, mkumbuke kutoa misaada katika jamii sio katika photocopy tu mnaweza kujenga hata shule utakuwa msaada mkubwa kwa jamii” amesema Mtaka.
Aidha Mtaka amesema bado jamii ya Dodoma haijawa na muamuko mkubwa kwenye suala la elimu wazazi wengi hawapeleki watoto shule mpaka kutumia nguvu ndipo wazazi wanawapeleka watoto wao shule.
“Niombe mtumishi wa Mungu mnapokemea mapepo pia mkemee mapepo ya uvivu, uzembe na pepo la kupokupenda elimu kwani elimu ndio kila kitu katika maisha” amesema.
Ameongeza kuwa “ Nikushukuru Mtumishi wa Mungu watenda kazi wake walipokuja ofisini kwangu niliwaomba kwamba mtusaidie katika jambo hili na nina shukuru ulilipokea na hatimae leo tumekabidhiwa kifaa hiki niombe na wengine waige mfano huu changamoto bado nyingi” amesema Mtaka.
Kwa upande wake Nabii Samweli Rolinga akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine hiyo amesema atahakikisha anashirikiana na jamii kwa kutatua changamoto zilizopo katika jamii na sio kuhubiri tu neno la Mungu.
“Kwa kweli Mkuu wa Mkoa umenifumbua jamii zuri sana na linalobariki mwanzo nilijikita tu katika kukemea mapepo lakini nimeona jambo hili ni jema kabisa na ninakuahidi jambo hili tutaliendeleza na tutafanya mambo makubwa zaidi” amesema Nabii Rolinga.
Amesema anatambua kuwa jamii inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kijamii na atahakikisha anashirikiana na jamii katika kuzitatua hasa kero kubwa ya maji ambayo ni changamoto katika maeneo mbalimbali.
Aidha Nabii Rolinga amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika kutoa elimu bure kutoka ngazi ya awali hadi kidato cha sita na ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika juhudi kubwa inazofanya.
Amewatoa wasiwasi wanafunzi wanaopitia katika mazingira magumu katika masomo yao na wasikatishwe tama na wanafunzi wanaotoka katika familia zinazojiweza kwani matokeo ya mwisho ndio yatakayoamua.
Nae Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dodoma mwalimu Francis Wambura ameshukuru kwa msaada huo kwani utakwenda kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili na itakuwa chachu kwa wanafunzi kujisomea hasa katika mitihani.