wa jimbo la Mafinga MjiniCosato Chumi akiongea na wananchi wa jimbo hilo wakati wa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya
kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.Mbunge
wa jimbo la Mafinga MjiniCosato Chumi akiongea na wananchi wa jimbo hilo wakati wa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya
kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.
Baadhi ya mabango yakionesha nini kimefanyaika jimbo la mafinga Mjini
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya
kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge
wa jimbo la Mafinga Mjini amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya
kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumza
wakati wa kongamano la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambalo lilikuwa
limeandaliwa na wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini,mbunge Cosato Chumi alisema
kuwa serikali ya awamu ya sita imetoa fedha nyingi kwenye miradi ya kimaendeleo
katika jimbo hilo.
Chumi
alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imefanikisha kuwatua ndoo akinamama
baada ya kuwapelekea miradi mingi ya maji ambayo ndio itakuwa inatatua
changamoto ya maji ambayo imekuwa ikiwatesa wananchi wa jimbo hilo.
Alisema
kuwa jimbo la Mafinga limepatiwa kiasi cha shilingi bilionni 58 kwa ajili ya
mradi wa maji ambao utasaidia kuongezeka kwa upatikanaji wa maji ya uhakikia
kwa wananchi wote wa jimbo la mafinga
“Kazi ya mbunge sio kwenda
kuizodoa Serekali bungeni,Bali ni kuchukua maoni na changamoto zinazogusa
maisha ya watu na kwenda kujenga hoja bungeni ili kuweza kupata ufumbuzi na
mwarubaini wa changamoto za watu wako ” Chumi
Chumi alimpongeza
waziri wa Nishati Januari Makamba kwa serikali kusitisha zoezi la uagizaji
nguzo kutoka njee ya nchii,iliyozua sitofahamu na taharuki , kwani Jambo hilo
lilikuwa linaenda kuuwa uchumi wa watu wengi.
Alisema
kuwa maamuzi ya serikali yamekuwa na manufaa kwa wananchi wa mikoa ya
Iringa,Njombe na Tanga ambako ndio haswa wanazalisha nguzo za umeme na kuongeza
ajira kwa wananchi ambao wapo kwenye sekta ya misitu.
Chumi alimpengeza
rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi
kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa taifa na wilaya ya Mufindi hasa pale
alipoamua kutenga bajeti ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Mafinga
,mgololo,Nyololo ambayo sasa itachochea kukua kwa uchumi kwa wananchi wa wilaya
hiyo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Daud yassin
alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madarasa katika shule zote za wilaya hiyo.
Yassin
alisema kuwa fedha za UVIKO 19 zilisaidia katika ujenzi wa madarasa na
kuwapunguzia michango kwa wananchi wote wa watanzania.
Alisema
kuwa wilaya ya Mufindi imenufaika na fedha kwenye miradi ya elimu na afya
ambayo hapo awali ilikuwa ngumu sana kupata fedha hizo kwenye miradi
mbalimbali.
Yassin
alisema kuwa katika bunge la bajeti la mwaka wa 2022/2023 wamepewa ujenzi wa
barabara ya Mafinga mgororo ambayo ilikuwa kilio kwa wananchi wa wilaya ya
Mufindi kwa ajili ya kukuza uchumi.
Alisema
kuwa kwa kiasi kikubwa uchumi wa wananchi wa Mufindi unategemea barabara hiyo
ambayo imekuwa ikipitisha bidhaa mbalimbali za mazao ya misitu ambayo ndio
kitovu cha uchumi kwa wanamufindi wote.
Yassin
alimazia kwa kusema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi wanafanya
kazi kwa ushirikiano mzuri na serikali ya wilaya ndio maana kimekuwa na
mafanikio makubwa ya kimaendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
kimaendeleo.