Na Silvia Mchuruza,Bukoba.
Waalimu katika manispaa ya bukoba mkoani kagera wameiomba serikali ya wilaya na na wadau kwa jumla kupewa mafunzo ya masuala ya watu wenye ulemavu ili kuweza kuwatambua watoto wenye ulemavu ambao wanatakiwa kuwa katika kitngo cha elimu jumuishi katika shule zao.
Akizungumza na kcr fm ofisini kwake mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi kashabo mwl.Gidio Ferix Kinjoy amesema shule iyo ina kitengo cha elimu jumuishi lakini bado walimu awajatambua wanafunzi hao kwa asilimia mia ambao wana ulemavu kwani uleemavu upo wa aina mbalimbali.
”kiukweli hapa shuleni hapa bado walimu awajawa na uelewa wa elimu jumuishi na kuweza kuwatambua wanafunzi wenye ulemavu na hao waliotambuliwa 15 ni kutokana nasemina ambayo niliipata mimi nawalimu wenzangu watatu kutoka kwa wadau wa elimu jumuishi likiwemo shirika la Tekla Kagera ambalo kidogo lilitupa mwanaga na tukaweza kuwatambua watoto hawa.
Aidha ameongeza kuwa mpaka sasa shule hiyo inao wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbalimbali wapatao 15 kuanzia darasa la awali mpa darasa la saba na hao walitambuliwa kutoka na semina walio ipata baadhi ya walimu akiwemo na yeye pia kutoka katika shilika la tekra kagera .
Pia ameelezea changamoto zinazowakabili kwa asilimia kubwa shuleni hapo ni kutokuwepo kwa uelewa zaidi kwa walimu juu ya elimu jumuishi ya kuweza kuwatambua wanafunzi wenye ulemvu kwani wengine wana ulemavu uliojificha