Naibu Mkaguzi Mkuu, Bw. Benjamini Mashauri akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Kijiji cha Matumaini, Sr. Maria Rosaria Gargiulo. Msaada huo umetolewa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ikiwa sehemu ya kutekeleza utaratibu wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2022 kwa malengo ya kujenga mahusiano mazuri na jamii.
Naibu Mkaguzi Mkuu, Bw. Benjamini Mashauri na Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bi. Sakina Mfinanga wakiwa na watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Matumaini mara baada ya kuwakabidhi msaada na zawadi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ikiwa sehemu ya kutekeleza utaratibu wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2022 kwa malengo ya kujenga mahusiano mazuri na jamii.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kutoka Divisheni na Vitengo mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wasimamizi wa Kituo cha Watoto cha Kijiji cha Matumaini mara baada ya kukabidhi msaada kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ikiwa sehemu ya kutekeleza utaratibu wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2022 kwa malengo ya kujenga mahusiano mazuri na jamii.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kutoka Divisheni na Vitengo mbalimbali wakisiliza taarifa ya huduma zinazotolewa na Kijiji cha Matumaini wakati walipotembelea Kituo kwa ajili ya kutoa misaada ya vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2022.
Wasimamizi na Watoto wa Kituo cha Kijiji cha Matumaini wakiimba kwa pamoja wimbo wa kuwakaribisha Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati walipowatembelea watoto hao ili kuwapa faraja pamoja na kutoa msaada wa vitu na zawadi mbalimbali kwa watoto hao. Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2022.
Naibu Mkaguzi Mkuu, Bw. Benjamini Mashauri akiwa na furaha na mmoja kati ya Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Yatima cha Kijiji cha Matumaini.
Mtumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bi. Upendo Ghanday akiwa amembeba kwa furaha watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto cha Kijiji cha Matumaini.
Mtumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bw. Baraka Mahenge akiwa amembeba kwa furaha watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto cha Kijiji cha Matumaini.
Mtumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bw. Benedict Sailes akiwa amembeba kwa furaha watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto cha Kijiji cha Matumaini.
Mtumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bi. Zuhura Rajab akiwa amembeba kwa furaha watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto cha Kijiji cha Matumaini.
Mtumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bi. Joseline Kashura akiwa amembeba kwa furaha mmoja kati ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha Watoto cha Kijiji cha Matumaini.
Mtumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bi. Upendo Ghanday akigawa zawadi kwa watoto wa kituo cha Watoto cha Kijiji cha Matumaini.
Naibu Mkaguzi Mkuu, Bw. Benjamini Mashauri akitoa mchango wa kuwezesha harambe fupi ambayo iliendeshwa Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuchangia Kituo cha Kijiji cha Matumaini ambapo fedha zilizochangwa na Watumishi zilikabidhiwa kwa Kituo.
Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakifurahia jambo na Watoto wa Kijiji cha Matumaini mara baada ya Wafanyakazi hao kufika katika kituo ili kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2022.
……………………………………
Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) wamekabidhi msaada kwa kituo cha watoto yatima kilichopo Kijiji cha Matumaini jijini Dodoma. Msaada huo umekabidhiwa kwa mlezi wa Kituo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa mwezi Juni kila mwaka.
Akizungumza kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – Divisheni Serikali za Mitaa, Bw. Benjamin Mashauri amesema utoaji wa msaada huo ni sehemu ya hatua mbalimbali zilizopendekezwa katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2022.
“Kwa namna ya pekee naomba upokee salamu za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ambae anatambua kazi kubwa mnayoifanya katika kituo hiki ya kulea watoto na Ofisi yetu itaendelea kutoa misaada kwa jamii kadri itakavyowezekana,” amefafanua zaidi Mashauri. Msaada uliotolewa kwa kituo ni pamoja na mchele, sukari, maji ya kunywa, maziwa ya unga aina ya lacktojeni kwa watoto wachanga, sabuni za kufulia, sabuni za kuogea, mafuta ya kupikia, soda, juisi na zawadi nyingine za kuwapa watoto faraja.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ni moja ya matukio muhimu katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kufanya maonyesho ya kazi mbalimbali na Kongamano kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma. Moja kati ya shughuli zilizotekelezwa katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka huu ilikuwa ni pamoja na kufanya shughuli za kijamii ili kujenga mahusiano mazuri na Wananchi.
Kwa kutambua kwamba Kijiji cha Matumaini kinatoa mchango mkubwa katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha ustawi wa jamii hususani katika kulea na kutunza watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu. Mbali na kukabidhi msaada huo wa Ofisi, Wafanyakazi walioshiriki kwenye tukio hilo waliendesha harambee fupi na kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni 1 na laki 4 ambazo walizikabidhi kwa Kituo ili ziweze kusaidia mahitaji ya Kituo.