Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bw. Elias Ntiruhungwa, wakizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi katika ya TMDA na wafamasia wa Halmshauri za Mkoa wa Mtwara. |
Meneja wa TMDA-Kanda ya Kusini, Engelbert Bilashoboka Mbekenga, wakizungumza na wakaguzi kutoka TMDA na Halmashauri za Mkoa wa Mtwara, wakati wa kikao kazi |
Wakaguzi wakifuatilia mada ambazo zilikuwa zinawasilishwa kutoka TMDA, katika kikao kazi kilichoshirikisha wakaguzi wa TMDA na wa Halmashauri wa Mkoa wa Mtwara |
Bw. Nassoro Juma, Mfamasia wa Mkoa wa Mtwara, wakitoa neno la shukrani kwa niaba wa wakaguzi wengine kwenye kikao kazi |
Na Mwandishi wetu Mtwara
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Kanda ya Kusini imefanya kikao kazi na wafamasia wa halmashauri za Wilaya ya Mkoa wa Mtwara, kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Halmashauri hizo ni Mtwara Manispaa, Wilaya ya Tandahimba, Wilaya ya Newala, Wilaya ya Masasi, Masasi Mji, Newala Mji, Wilaya ya Nanyumbu na Wilaya Nanyamba.
Kikao kazi hiki kimefunguliwa na Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bw. Elias Ntiruhungwa, alielezea fedha zilizotumika kuandaa kikao kazi hiki ni fedha za wananchi kwa hiyo watumie vizuri kikao hiki kwa kile watakachokipata hapa kiwe chachu ya kuwatumikia wananchi kwa ufanisi mkubwa kwani wanadhamana ya kulinda jamii.
Mgeni Rasmi, alishukuru kwa kufahamishwa tumbaku na bidhaa zake zimepata mthibiti amesema
Kwa muda mrefu zao hili zimekuwa halina mthibiti, hali itakayopelekea kuwa na mipango endelevu kuwezesha jamii kuelewa madhara ya tumbaku na bidhaa zake na namna gani kujilinda zaidi na madhara hayo
Lengo mahususi la Kikao kazi hiki ni kukumbushana kazi ambazo zinafanywa na TMDA, ambazo wamekasimishwa Halmashauri katika kusaidia kufanya kazi hizo kwa weledi, kazi hizo ni kufanya ukaguzi kwenye maeneo yanayotoa huduma za afya kama maduka ya dawa, maabara, zahanati, vituo vya afya na hospitali lengo likiwa ni kuangalia usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa upande wa binadamu na mifugo.
Kikao kazi hiki kiliongozwa na Meneja TMDA Kanda ya Kusini, Dkt. Engelbert Bilashoboka Mbekenga, ambaye aliwasii wakaguzi kuwa watiifu katika kazi zao kwani kazi yao ni ngumu na inahitaji utiifu katika kulinda afya ya jamii.
Katika hitimisho la kikao kazi hicho, Mganga Mkuu wa Mji Masasi, Dkt.Salum Gembe ambaye alishukuru Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, Kanda ya Kusini kwa kuliona hili la kuwajengea uwezo kwa mara nyingine wakaguzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mtwara, ambayo itawezesha wafamasia kuongeza weledi kwenye kutekeleza majukumu yao pamoja na majukumu ambayo yamekasimishwa na TMDA kwenye Halmashauri zao.
Pia alishukuru kusikia kuna changamoto ya utekelezaji wa majukumu ambayo yamekasimishwa na TMDA, amesema ameyachukua na ameshawasilisha kwenye umoja wa waganga wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mtwara kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kutekelezeka kwa wakati.
Na kwa suala la kuwa na taarifa chache wa madhara yanayohisiwa kusababishwa na matumizi ya dawa, vifaa tiba na chanjo amelichukua na kuona namna gani taarifa hizi zinapatikana na kuwasilishwa TMDA.