Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian akisistiza jambo mbele ya madiwani wilayani nzega.
Baadhi wa madiwani wakishiriki kikao cha baraza hilo wilaya humu
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauriya wilaya ya Nzega, Kiomoni Kibamba akisisitioza jambo mbele ya baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya nzega
……………………………………..
Na Lucas Raphael,Tabora
Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkonia Tabora imetakiwa kuwasilisha Makato ya mishahara kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii PSSSF ambayo haya kuwasilishwa kiasi cha shilingi milioni 104,686,299 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian wakati wa Baraza maalumu la madiwani kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Alisema kwamba licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi lakini fedha za watumishi zinapaswa kuwasilishwa kwenye eneo husika ili kuepusha usumbufu na adhabu zisizo na msingi.
“Katika hoja hii naelekeza halmashauri kupeleka makato PSSSF kwa wakati ili kuepuka adhabu ya matumizi ya Fedha yasiyokuwa na faida”alisema Balozi Dkt Batilda .
Alisema kwamba fedha za makato ya wafanyakazi ni ni haki yao kuwasilishwa kwenye mifuko ya jamii ili iweze kunufaisha watumishi hao mara baada ya kumaliza utumishi wao.
Katika hatua nyingne Mkuu huyo wa mkoa wa Tabora amemtaka mkurungezi wa halmashauri ya wilaya ya nzega Kiomoni Kibamba kuwachukulia hatua za kisheria vikundi vitakavyokaidi kurejesha fedha walizokopa ikiwemo wakuwafikisha mahakamani.
Balozi Dkt Batilda alisema kwamba Kutokurejeshwa kwa mikopo ya asilimia 10 iliyotolewa kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ni kufifisha juhudi za halmashauri na serikaliya mkoa .
Alisema kwamba fedha hizo ni kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita kiasi cha shilingi milioni 145,133,500.00 kitu kinachorudisha nyuma jitiada za serikali kuhakikisha kundi kubwa la watu wanapatiwa mikopo hiyo .
“Naomba nipewe mpango mkakati wa jinsi fedha hizi zitarejeshwa ili waweze kukopeshwa makundi mengine kwani uhitaji ni kubwa sana wa mikopo hiyo”alisema Balozi Dkt Batilda
Halmashauri ya wlaya ya Nzega mkoani hapa kwa mwaka wa Fedha 2020/21, imepata hati safi imetokana na kuzingatiwa kwa viwango vya Uhasibu vya Kimataifa vya uandaaji wa taarifa za Fedha katika Taasisi za Umma (IPSAS).