Na Silvia Mchuruza,Bukoba.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba BUWASA, imekamilisha ahadi yake ya utoaji utoaji wa computer katika shule ya sekondari kashai iliyopo manispaa ya Bukoba mkoani kagera.
Computer hiyo imekabidhiwa na mkurugenzi wa maji BUWASA Ndg. John Sirat pJune 22 mwaka huu ikiwa Ni sehemu ya kutimiza ahadi yake katika shule hiyo aliyoitoa katika maafari ya mwaka Jana.
Aidha ndg. Sirat amesema katika kuhakikisha uboreshaji wa huduma ya upatikanaji wa Maji Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba BUWASA imedhamilia kufungua club za Maji katika shule mbalimbali za Manispaa ya Bukoba.
Sirati amesema kuwa Mamlaka imekuwa ikikabiriwa na changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya Maji, ambapo amesema kuwa kuanzishwa kwa club hizo mashuleni kutaongeza mabalozi wazuri watakao weza kulinda na kutoa Taarifa pale watakapoona uharibifu wa miundombinu ya maji katika maeneo yao.