WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Innocent Bashungwa,akizungumza leo Juni 21,2022 jijini Dodoma na watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),anayeshughulikia Elimu David Silinde,akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)anayeshughulikia Afya,Mhe. Dk. Festo Dugange,akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ,akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe,akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
SEHEMU ya Watumishi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Innocent Bashungwa (hayupo pichani),awakati akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Innocent Bashungwa,akiwa katika picha ya pamoja na watumishi mara baada ya kuzungumza nao ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
…………………………………….
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa,amewataka watumishi wa Wizara yake kutoshiriki kwenye vitendo vya rushwa pamoja na kughushi barua za uhamisho wa watumishi.
Hayo ameyasema leo Juni 21,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo huadhimishwa Juni 16 hadi 23 kila mwaka.
Waziri Bashungwa amesema suala hilo kwa watumishi wa Wizara yake si hiyari bali ni lazima kujiepusha na vitendo vya rushwa.
” Sisi tunafanya kazi Ofisi ya Rais ni lazima tulinde taswira na heshima ya Ofisi ya Rais, suala la rushwa halikubaliki, hivyo tukatae, tukemee na tupambane na vita dhidi ya rushwa na kufanya hivyo tutalita heshima ya ofisi ya Rais.”amesema Bashungwa
Hata hivyo amewataka watumishi hao kutoshiriki kwenye vitendo vya hovyo ikiwemo kushiriki katika kugushi barua za uhamisho wa watumishi.
“Watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI wanawajibu wa kutunza siri za Serikali kama maelekezo ya viongozi wa juu na hasa ikizingatiwa kuwa asilimia 70 ya watumishi wa umma wanatoka TAMISEMI,”amesisitiza
Pia Waziri Bashungwa,amemshukuru Rais Samia kwa kutoa nyongeza sa mshahara na kusisitiza kuwa nyongeza hiyo kwa sehemu kubwa inakwenda kuwanufaisha watumishi kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo inasailimia 70 ya watumishi wa umma.
Kwa upande wake Naibu waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde,amewataka watumishi hao kila mmoja anatekeleaa majukumu yake hasa kutokana na kuwa ni Ofisi inayohudumia wananchi moja kwa moja.
Naye Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Shemdoe,ameahidi kuwa atatekeleza maelekezo ya Waziri na kuwataka watumishi hao kuwa waadilifu.