Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha maafisa Elimu wa Halmashauri 33 ambako mradi wa CAMFED unatekelezwa walipokutana Juni 21,2022 jijini Dodoma kuona namna bora ya kuendelea na mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la CAMFED Bi. Lyidia Wilbad akizungumza wakati wa ufunguzi kikao kazi cha maafisa Elimu wa Halmashauri 33 ambako mradi wa CAMFED unatekelezwa walipokutana leo Juni 21,2022 jijini Dodoma kuona namna bora ya kuendelea na mradi huo.
Mkurugenzi wa Elimu kutoka OR TAMISEMI Mwalimu Ephraimu Simbeye akizungumza wakati wa ufunguzi kikao kazi cha maafisa Elimu wa Halmashauri 33 ambako mradi wa CAMFED unatekelezwa walipokutana Juni 21,2022 jijini Dodoma kuona namna bora ya kuendelea na mradi huo.
Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Sekondari kutoka OR TAMISEMI Bi. Hadija Mcheka, akizungumza wakati wa ufunguzi kikao kazi cha maafisa Elimu wa Halmashauri 33 ambako mradi wa CAMFED unatekelezwa walipokutana leo Juni 21,2022 jijini Dodoma kuona namna bora ya kuendelea na mradi huo.
Baadhi ya Maafisa Elimu kutoka Halmashauri 33 ambako mradi wa CAMFED unatelelezwa wakimsikiliza Katibu Mkuu OR TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi kikao kazi cha maafisa Elimu wa Halmashauri 33 ambako mradi wa CAMFED unatekelezwa walipokutana Juni 21,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe wa tatu kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha Maafisa Elimu wa Halmashauri 33 ambako mradi wa CAMFED unatekelezwa walipokutana leo Juni 21,2022 Dodoma.
……………………………………………
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amewaagiza Maafisa Elimu katika Mikoa, Wilaya na Halmashauri ambako ujenzi wa shule za wasichana kila mkoa zinajengwa kuhakikisha wanazingatia miundombinu ya kujisitili kwa wanafunzi wa kike wakati wa hedhi.
Pia amewataka kuhakikisha wana simamia kikamilifu miradi ya CAMFED inayotekelezwa na taasisi inayojishughulisha na kusaidia watoto wa kike kupata elimu mradi unaotekelezwa katika Halmashauri 33 hapa nchini.
Prof. Shemdoe ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Elimu wa Halmashauri 33 ambazo mradi wa CAMFED unatekelezwa waliokutana kwa lengo kujadili namna bora ya kuboresha utendaji kazi wa mradi huo.
Ambapo amesema kuna ujenzi wa shule 26 za wasichana ambapo kila mkoa itajengwa shule moja na kwa kuanza wanaanza na shule 10 katika mikoa 10 kupitia mradi wa SEQUIP.
“Kwa kutambua umuhimu wa kumlea mtoto wa kike wa Tanzania katika mazingira salama OR TAMISEMI na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia tunajenga shule 26 za wasichana kupitia mradi wa SEQUIP naagiza kila shule iwe na mazingira wezeshi kwa watoto wa kike kujisitiri” Amesema Prof. Shemdoe.
Pia amebainisha kupitia mradi huo watoto wa kike walioachishwa masomo kwa sababu mbalimbali wamerejeshwa shule ndani ya miaka miwili na kuendelea na masomo katika mfumo rasmi na nje ya mfumo yote hayo ni katika kuweka mazingira mazuri kwa mtoto wa kike kupata masomo.
Akizungumzia mradi wa CAMFED Prof. Shemdoe amesema mradi huo umekuwa mkombozi mkubwa kwa watoto wa kike kupata elimu hasa wale wanaotoka katika familia zisizojiweza ambao kupitia mradi huo watoto hao wanawezeshwa mahitaji mbalimbali na hatimaye kuendelea na masomo.
“Napenda kuwashukuru CAMFED kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika nchi yetu mnasaidia kutekeleza vipaumbele vya serikali kuhakikisha watoto hususa ni watoto wa kike wanapata elimu kwa kuwasaidia katika nyanja mbalimbali” amesema.
Aidha amezitaka Halmashauri 33 ambako mradi huo unatekelezwa kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha watoto wa kike wanaopatikana katika maeneo hayo wananufaika na mradi huo na hatimaye kuendelea na masomo.
“Nimejulishwa kuwa malengo mahususi ya kikao hiki ni kujadili juu ya kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kati ya Serikali na shirika la CAMFED kwa kuangalia ni jinsi gani mradi ulioanzishwa na CAMFED inaweza kufanyika kwa ufanisi hata pindi mradi huo utakapoacha kufanya kazi lakini kazi hizo ziendelee” amesema.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la CAMFED Bi. Lyidia Wilbard amesema shirika hilo linajishughulisha na kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu kwa kuondoa baadhi ya vikwazo wanavyokutana navyo hasa kwa watoto wanaotoka familia maskini kuweza kuendelea na masomo.
Amesema miongoni mwa vitu wanavyowasaidia watoto wa kike kuwawezesha kuendelea na elimu ni kuwawezesha kupata sare za shule na vifaa vingine vinavyotakiwa kwa wanafunzi kuwepo shule kwa muda wote na wanaosaidiwa ni wale wanaotoka kaya maskini.
“Tunaishukuru serikali kwa juhudi kubwa wanazofanya hasa kwa kuondoa ada hali ambayo imesaidia watoto wengi kuandikishwa shuleni na kuendelea na masomo hasa kwa wale waliokuwa hawaendi shule kwa kukosa ada” amesema Bi. Lyidia.
Amesema Shirika limejikita katika kusaidia watoto wa maskini wakiamini ya kuwa watoto wa kike wakipata elimu hata wakija kupata watoto wao lazima watahakikisha watoto wao nao wanapata elimu hivyo wanaamini watakuwa wamekomboa kizazi chake.
Amesema mpaka sasa wamezifikia shule za Sekondari zaidi ya 490 na shule za msingi zaidi ya 360 katika halmashauri 33 ambazo wamezifikia kwa kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu ambapo wengi wangeweza kushindwa kupata elimu.
Amesema watoto wengi ambao wamewezeshwa pia wamekuwa wakiingia katika kamati za uongozi katika ngazi mbalimbali ambapo wanaamini wanawajengea watoto hao wa kike kujiamini na kupata nafasi mbalimbali za uongozi.