Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe
Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha inasimamia Marejesho ya kiasi cha sh. Milioni 473 ,ambazo ni makusanyo ya fedha za ndani zilizokusanywa na kutokupelekwa Benki hali iliyosababisha kupata hati ya Ukaguzi yenye mashaka.
Vilevile, ameiagiza kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale walioshiriki kuchukua fedha hizo na kuisababishia hasara Halmashauri hiyo.
Kunenge alitoa agizo wakati alipohutubia kikao maalum cha Baraza la madiwani ,kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kilichokaa kupitia na kujadili Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mwaka 2020/2021.
“Ni kwanini Wameacha mpaka haya yakatokea, Wataalam hamkufanya Wajibu wenu” Kuna wakati Kuna fanyika upuuziaji wa makusudi”Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri aliwashauri lakini hamkuchukua hatua, Mkaguzi wa Ndani alifanya kazi nzuri”
“Maagizo yangu Fedha Shilingi Milioni 473 hizo zirudi ifakapo Septemba 2022 na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote waliosababisha haya “Alisisitiza Kunenge.
Nae Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoani Pwani ,Mary Dibogo aliitaka halmashauri hiyo kutoa ushirikiano pindi wanapokuja kufanya ukaguzi kwani hii itasaidia kuondoa kasoro ndogo ndogo zinazopelekea kupata hati yenye mashaka
Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG ya mwaka wa fedha 2020/2021 ilieleza kuwa Halmashauri ya kisarawe ilikuwa na Hoja 39 kati ya hizo 15 zimefutwa na 24 hazijapata majibu na kati hizo hoja 6 tu ndio zipo ndani ya uwezo wao.