Makamu Mwenyekiti Chama cha Walemavu
Tanzania (CHAWATA) mkoa wa Iringa Leo Sambala akiongea wakati wa
mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali uliondaliwa na shirika lisilo
la kiserikali la IDYDC na kufadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali
linalotekeleza mradi wa Inclusive Media Project unaofadhiliwa na
Internews Tanzania
Na Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA
cha walemavu mkoa wa Iringa kimeiomba Serikali kuwapatia upendeleo wa ajira
pindi zinvyotangazwa ili nao waweze kupata ajira hizo kwa kuwa wanauwezo wa
kufanya kazi kama watu wengine na itasaidia kutatua changamoto ya kukosekana kwa
ajira kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari Makamu
mwenyekiti chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA),Iringa Rukia Makweta alisema
kuwa moja ya adhima nzima za elimu jumuishi ni kuanda taifa la watu wenye
mahitaji maalaumu na walemavu ambao si tegemezi kwa kuwaandaa kujiajiri na
kuajiriwa.
Makweta alisema kuwa muda mrefu nchini
Tanzania kumekuwa na dhana kuwa mlemavu ni mtu anayepaswa kuwa tegemezi katika
jamii jambo ambalo si kweli.
Alisema kuwa
baadhi ya watu huenda mbali zaidi na kuwaficha watu wenye ulemavu ili
wasionekane na jamii kiasi cha kuwakosesha fursa za kijamii na kiuchumi ikiwemo
elimu na mitaji,ajira.
Makweta alisema kuwa licha ya kuwa nyuma
katika fursa mbalimbali kutokana na mitazamo hasi ya jamii dhidi yao, idadi ya
watu wenye ulemavu wanaojitosa katika shughuli za kiuchumi Tanzania imezidi
kuongezeka kwa kasi ndani ya miaka saba iliyopita.
Kwa upande
wake Katibu wa wa shirikala watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) mkoa wa
Iringa Leo Sambala alisema kuwa ripoti ya
utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ya mwaka 2020/21 iliyotolewa na
Ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS), inabainisha kuwa idadi ya watu wenye ulemavu
wenye ajira imeongezeka hadi takriban theluthi mbili au asilimia 63.2 mwaka
2020/21 kutoka asilimia 59.1 mwaka 2014.
Sambala alisema
kuwa inamaanisha hadi mwaka jana takriban watu sita kati ya 10 wenye ulemavu
walikuwa na ajira ama kwa kujiajiri au kuajiariwa.
Katika
kipindi hicho, kiwango cha watu wenye ulemavu wenye umri miaka 15 na zaidi
ambao hawakuwa na ajira nacho kilishuka. Takwimu hizo zinaeleza zaidi kiwango cha watu wenye ulemavu mwaka
2020/21 kilikuwa asilimia 6,nusu ya kile kilichokuwepo mwaka 2014 ambacho
kilikuwa asilimia 12.4.
Kwa nyakati tofauti serikali imekua inawahamasisha walemavu kuchangamkia fursa za
ajira zinazotangazwa na serikali kwa sababu ni wachache wanaojitokeza
ikiashiria Mwamko mdogo wa walemavu
katika uombaji wa ajira.serikali inasisitiza kwamba endapo mtu mwenye ulemavu au mahitaji maalumu atakua
ametimiza vigezo bila kuogopa changamoto zinazowakabili kuomba ajira hizo kwani
mchakato wote wa maombi ya ajira unafanywa kwa kufuata kanuni na Sheria za Nchi
ambayo inampa kila mtu haki ya kupata ajira,
Alisema kuwa sheria namba 9 ya Ajira ya mwaka 2010
inasema,“Mwajiri yoyote awe wa Umma au Binafsi mwenye waajiriwa kuanzia 20 na
kuendelea lazima asilimia 3 ya waajiriwa hao iwe kwa ajili ya watu wenye
ulemavu” hii inaonyesha kuwa walemavu wana haki ya kuajiriwa mahali popote.
Lakini Sambala alisema kuwa ni vyema walemavu
kuzitaja changamoto zao kweye fomu za maombi ili serikali iweze kuwaandalia
mazingira rafiki kwa ajili ya mchakato mzima wa upatikanaji wa ajira na baada
ya kupata ajira waweze kupangiwa sehemu ambazo hazitakua changamoto kwao.
Aidha Serikali inawapa kipaumbele walemavu kuanzia
wakati mchakato wa usajili hadi wakati wa kupanga ajira hivyo basi walemavu
wenye vigezo vilivyoanishwa kwenye matangazo ya ajira wajitokeze kutuma maombi
ya nafasi hizo.
Walemavu wanahaki kisheria hivyo waachane na mawazo
ya kudhani wakitaja changamoto zao kwenye maombi hawatapatiwa nafasi.
Sambala alisema kuwa Serikali inatambua nafasi ya
Walemavu katika kuchangia maendeleo ya Nchi na ina wahamasisha kutumia fursa
mbalimbali zinazojitokeza ili kujikwamua kiuchumi.
katika kutambua umuhimu wa vyombo vya habari
Iringa Development of youth disabled and children care(IDYDC)
shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa Inclusive Media
Project unaofadhiliwa na internew
Tanzania katika mkoa wa Iringa kupitia
Mratibu wa mradi Reuben Magayane alisema
kuwa vyombo vya habari vinapaswa kusema kuwasemea watu wenye ulemavu ili waweze
kuapata ajira kama watu wengine.
Magayane alisema kuwa waandishi wa habari na
vyombo vya habari vinaweza kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kufikisha ujumbe
moja kwa moja kwa serikali husika.