Baadhi ya viongozi wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Iringa na wadau wa watu wenye ulemavu wakiwa kwenye mafunzo maalamu ya elimu jumuishi.
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA
cha walemavu mkoa wa Iringa kimeiomba Serikali kutatua changamoto ya kukosekana
kwa miundombini bora ya wanafunzi wenye ulemavu ili nao waweze kupata elimu
kama wanafunzi wengine wasio na ulemavu.
Akizungumza
wakati mkutano Makamu
mwenyekiti chama cha walemavu Tanzania(CHAWATA),Iringa Rukia Makweta alisema
kuwa mfumo wa elimu maalaumu unachangamoto nyingi ndiyo maana jamii imetakiwa
kufahamu umuhimu wa mfumo wa elimu jumuishi pamoja na kwamba miundombinu ni
changamoto kwao.
Makweta
alisema kuwa watoto wenye mahitaji maalumu kuchanganyikana na wengine
inatengeneza umoja na kuondoa unyanyapaa kwa kuwa tayari wamezoeana na
kupendana pamoja na kupewa ushirikiano kutoka kwa wenzao.
“Nafikiria
itakuwaje mwanangu atakapoanza masomo? Mazingira hasa ya vyoo kwenye shule
nyingi hasa hapa kijijini hayaruhusu mlemavu kusoma, ni bora nibaki nae
nyumbani,” Alisema
Makweta
alisema kuwa sehemu kubwa ya jamii nchini imeendelea kukumbatia utamaduni wa
kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwa madai mbalimbali ikiwamo ya kuhofia
aibu au kuwaona hawatakuwa na uwezo wa kushiriki shughuli za kijamii ikiwamo
elimu.
Alisema
kuwa hata kuwa Wilaya ya Iringa Kwa muda mrefu kumekuwa na kampeni
mbalimbali kuhusu watu wenye ulemavu hasa juu ya haki zao za msingi ikiwamo
elimu.
Makweta
alisema kuwa pamoja na kampeni hizo, bado kilio cha watu wenye ulemavu kupata
mahitaji yao muhimu ili waishi kama makundi mengine kwenye jamii hakikomi na
bado Kuna changamoto lukuki ikiwamo miundombinu isiyo rafiki kwa wanafunzi
wanaoishi na ulemavu, ni moja ya vilio vinavyowafanya baadhi kushindwa kupata
elimu.
Mkoa
Iringa ni kati ya mikoa inayokabiliwa na changamoto nyingi katika utoaji wa
elimu jumuishi kubwa ikiwa miundombinu isiyo rafiki.
Alisema
kuwa baadhi ya wazazi wanasema changamoto hizo ndiyo sababu kwa baadhi yao
kushindwa kuwapeleka watoto shuleni.
Nae Leo
sambala Katibu wa wa shirikala watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) mkoa wa
Iringa alisema miundombinu isiyo rafiki kwenye shule nyingi za msingi na
sekondari ni kati ya vikwazo vinavyoikabili elimu hiyo mkoani hapo.
Alisema
kama suala la miundombinu halitapewa uzito, watoto hao watashindwa kujifunza
ipasavyo.
“Ni kweli
shule zetu zinakabiliwa na miundombinu isiyo rafiki, hakuna vifaa vya
kujifunzia hasa kwa walemavu wasioona, hapa hakuna kujifunza,” anasema na
kuongeza;
Sambala
alisema kuwa Walemavu wa kutoona wanahitaji vifaa maalum ambavyo sio kila shule
inavyo, kwa hiyo huyu hatajifunza kama ataingia darasani na kukosa vifaa
hivyo.”
Kephason
ni mwanafunzi mwenye ulemavu wa kuona alisema shule jumuishi anayosoma
bado ina changamoto za kimiundombinu na kupelekea kuwa na ugumu kutoka
sehemu moja hadi nyengine awapo kwenye mazingira ya shule na kupelekea
kukosa ari ya kuendelea na masomo kama wanafunzi wengine na kuitaka serikali
kufanya jitihada madhubuti kurekebisha hili kwani kwa mwenendo huu wanafunzi
wengi wenye ulemavu wanaamua kuacha shule ili kuepukana na changamoto za
kimiundombinu wanazokutana nzao mashuleni kwani huwaathiri kisaikolojia.
Alisema
kuwa elimu jumuishi imepewa kipaumbele zaidi kuliko aina nyingine na
inachukuliwa kama njia bora
Mwalimu
wa shule ya msingi ambao inatoa elimu jumuishi, John Kijazi alisema kwa
mfano watoto wenye ulemavu wa miguu, wao wanakabiliwa na uhaba wa
vibaiskeli, jambo linalowafanya washindwe kujifunza ipasavyo.ili mtoto mwenye
ulemavu wa viungo apate elimu bora lazima awe na uhakika wa kutoka hatua moja
hadi nyingine kwa baiskeli.
Kijazi
alisema kuwa miundombinu kwa watoto wenye ulemavu bado ni shida wanahitaji
madarasa, walimu wa kutosha, mazingira rafiki ili kupata elimu bora.
Alisema
kuwa bado kuna changamoto kubwa hasa kutokana na kuwa na walimu wachache,
madarasa na mitaala isiyo rafiki kwa wanafunzi viziwi.
Kijazi
alisema kuwa hili ni kundi lililosahaulika hivyo juhudi binafsi zinahitajika
kwa wadau wote wa elimu kuhakikisha watoto hao wanapata elimu bora
Christopher
Hinju Afisa wa elimu maalum Iringa Hinju alisema kuwa Serikali imeahidi kuwa
itawaajiri walimu zaidi wa kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiwemo
wenye uziwi
Kwa
upande wake mratibu wa mradi wa elimu jumuishi kutoka shirika lisilo la
kiserikali la Iringa Development of youth disabled and children care
(IDYDC) shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa
Inclusive Media Project unaofadhiliwa na Internew Tanzania katika
mkoa wa Iringa kupitia Mratibu wa mradi Reuben Magayane katika kikao cha
kimkakati kilichohusisha wadau wa elimu na waandishi wa habari amesema lengo la
mradi ni kutumia vyombo vya habari kupaza sauti juu ya elimu jumuishi na
kuibua maswala ya makundi maalumu na walemavu kupitia vyombo vya habari jambo
ambalo limekuwa halipewi kipaumbele kwenye vyombo vya habari huku ikiiasa jitihada
jumuishi kutoka kwa waandishi wa habari,jamii na serikai ili kufikia lengo la
elimu kwani Msingi wa mafunzo mbalimbali katika jamii ni chachu ya kuondoa
mawazo mgando juu ya watu wenye mahitaji maalumu kuwa hawawezi,
Magayane
alisema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kutoa ushirikiano hitajika kwa watu
wenye mahitaji maalumu hasa katika upande wa elimu.
Na kwa
mujibu wa jarida ya Shirika la Kuhudumia watoto Duniani (Unicef) , kati ya
watoto watano ni wawili tu wapo shuleni.Sheria namba tisa ya watu wenye ulemavu
ya mwaka 2010, inataka haki sawa kwa watu wenye ulemavu ikiwamo elimu, ajira,
nafasi za uongozi na kuboresha miundombinu.
Hata
hivyo, wengi wanakabiliana na miundombinu isiyorafiki ambayo ni kikwazo katika
upataji wa elimu