Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw.Emmanuel Mgonja akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa Future STEM Business Leaders unaosaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto kwenye jamii. Meneja wa Mradi wa Future STEM Business Leaders Bi.Josephine Sepeku akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo unaosaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto kwenye jamii.Meneja Biashara wa Dar Teknohama Business Incubator(DTBI), Bw.Elia kinshaga akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa Future STEM Business Leaders unaosaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto kwenye jamii. Mkuu wa Idara ya Fizikia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Nuru Mlyuka akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa Future STEM Business Leaders unaosaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto kwenye jamii. Mkuu wa ndaki ya sayansi asilia na ndaki ya sayansi bunifu kutoka Chuo cha Dar es Salaam ,Prof. Flora Magige akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa Future STEM Business Leaders unaosaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto kwenye jamii. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw.Emmanuel Mgonja akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi ambao wameshiriki katika uzinduzi wa Mradi wa Future STEM Business Leaders unaosaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto kwenye jamii.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Mradi wa Future STEM Business Leaders unaosaidia wanafunzi wa kidato cha tano na sita kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kutatua changamoto kwenye jamii umezinduliwa leo Juni 20,2022 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo shule 17 za Sekondari kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Arusha zinashiriki mradi huo wa kufanya sanyasi kuwa na uhalisia katika jamii na kuifanya biashara.
Akizunguumza wakati wa uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw.Emmanuel Mgonja amesema wameamua kutengeneza mazingira wezeshi ili wanasayasi wapate nafasi ya kushauriwa na kukuzwa na sayansi kuwa na tija kwenye jamii.
“Wanasayasi wengi hawana mawazo ya kibishara huwa wanavumbua tu kupitia program hii mtambua changamoto za jamii na kufanyia kazi na hivyo wazo kubadilika na kuwa na Suluhu”. Amesema Bw.Mgonja
Nae Meneja wa Mradi huo Bi.Josephine Sepeku, amesema Mradi huo uliofadhiliwa na Dar Teknohama Business Incubator(DTBI) unakuza na kujenga daraja kati ya sayansi na biashara kwa wanafunzi hao.
Amesema Mradi huo ulianza mwaka 2017 ambapo awali walianza na Shule tano za Dar es Salaam na hadi sasa Shule 10 za Mkoa wa Dar es Salaam zimeshiriki na Shule Saba za Mkoa wa Arusha ambapo wanatarajiwa kwenda mikoa mingine.
“Tulianza na hizo shule tano kwasababu tulitaka kujua hiki kitu kitasaidiaje jamii na mwitikio wake na tunaposema Tanzania ya viwanda tunaanzia hapa na hapa tunaleta uhalisia kwamba anapojifunza darasani alete katika mazingira,”Amesema Bi.Sepeku.