KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael ,akipokelewa na watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael ,akipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga,akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Francis Michael mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael,akizungumza na watumishi wa wizara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Utawala na Rasilimali Watu Bw.Moshi Kabengwa,akizungumza wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 20,2022 jijini Dodoma.
……………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Francis Michael,amepokelewa na watumishi wa Wizara hiyo huku akiwaahidi ushirikiano na kusimamia masuala yote yanayohusu elimu nchini.
Akiwasili leo Juni 20,2022 katika Ofisi yake Mpya Mji wa Kiserikali Mtumba Dodoma mara baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu hivi karibuni.
Dk.Michael ameomba ushirikiano kwa watumishi wa Wizara hiyo na wasimuangushe katika kusimamia wizara hiyo.
“Masuala ya watumishi hamtapata shida lakini usipotekeleza wajibu sitakuwa na mzaha, tufanye kazi kama timu,”amesema Dk.Michael
‘Najisikia kuwa nipo nyumbani kwa kitaaluma mimi ni mwalimu na ninajua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu hivyo kwa kushirikiana na watendaji wote naamini kuwa tutafikia malengo ila nataka kila mmoja afanye kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili tumsaidia Rais kutimiza maono yake.’amesema Dk.Michael
Aidha amesema kuwa atawasiliana na w Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kupata maeneo ambayo yanahitajika kuweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma kada hiyo ili kupunguza uhitaji uliopo .
“Mimi kama katibu mkuu nitapita kwenye mipango na malengo ya wizara ili kuhakikisha sitoki nje ya malengo yaliyopo na mnaona hivi karibuni tu Rais wetu Mhe.Samia amepitisha Elimu bure kwa kidato cha tano na sita kikubwa ni kulinda maono na ile ndoto njema ili kuifikisha Elimu ya Tanzania katika eneo salama “Amesema Dkt.Michael
Hata hivyo amesema kuwa moja ya mikakati yake ni kuendeleza mchakato wa kuboresha mitaala ya elimu sambamba na kuimarisha vyuo vya kati ili kuziba pengo la mahitaji ya taaluma na ujuzi yaliyopo.
“Najua Wizara ya Utumishi imefanya uchambuzi kujua mapengo gani ya taaluma ambayo yanatakiwa ili kuziba na mitaala inatakiwa kulenga huko,”amesema Dk.Michael
Dk.Michael amesema kuwa atahakikisha anasaidia kutimiza malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye masuala ya elimu.
“Rais hivi karibuni amezungumza kuhusu masuala ya mapitio ya mitaala mambo hayo ni pamoja na yatakayonilenga mimi ninayopaswa kufanya,”amesema
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amemhakikishia ushirikiano mkubwa katibu huyo Mpya huku akisema kuwa watendaji wa wizara hiyo ni wachapa kazi hivyo atafurahia uwepo wake ndani ya timu hiyo mpya.
Kipanga amesema kuwa kuna haja ya kufanya kazi kama timu Iii kufikia malengo ya wizara na kuwatumika wananchi katika sekta ya elimu.
“Nakuhakikishia kuwa hapa ulipokuja ni kama nyumbani kwako na hawa unaowaona mbele yako ni majembe kweli kweli naongea hivyo nikiwa na uhakika mkubwa kuwa utafurahia uwepo wako hapa lakini naomba usituchoke sisi kuna muda tutahitaji documents naomba utusaidie kwa sababu ni katika hali ya kufanya mambo yakae sawa sawa” Amesema Kipanga