Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) upande wa Taaluma,Ushauri elekezi, Dkt Omary Moshi akizungumza hafla ya kuwajengea uwezo wahitimu wa mafunzo ya kozi mbalimbali katika Chuo hicho ili waweze kukabilina vyema na changamoto za ajira baada ya kuhitimu.Mkurugenzi wa (Research Publication and Postigraduate Studies) NIT, Dkt.Eva Luwavi akizungumza hafla ya kuwajengea uwezo wahitimu wa mafunzo ya kozi mbalimbali katika Chuo hicho ili waweze kukabilina vyema na changamoto za ajira baada ya kuhitimu. Mshauri wa Wanafunzi Ustawi wa Wanafunzi NIT, Bw.Meshack Kimaro akizungumza katika hafla ya kuwajengea uwezo wahitimu wa mafunzo ya kozi mbalimbali katika Chuo hicho ili waweze kukabilina vyema na changamoto za ajira baada ya kuhitimu. Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) katika hafla ya kuwajengea uwezo wahitimu wa mafunzo ya kozi mbalimbali katika Chuo hicho ili waweze kukabilina vyema na changamoto za ajira baada ya kuhitimu.
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Mashirika na Makampuni mbalimbali yameombwa kutoa nafasi za kujitolea kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali ili kuwapa fursa ya kupata uzoefu na kuwaandaa kuwa wafanyakazi bora.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) upande wa Taaluma,Ushauri elekezi, Dkt Omary Moshi wakati akizungumza katika hafla ya kuwajengea uwezo wahitimu wa mafunzo ya kozi mbalimbali katika Chuo hicho ili waweze kukabilina vyema na changamoto za ajira baada ya kuhitimu.
Amesema kuwa kwa sasa soko la ajira kwa sasa limezidi kuwa la ushindani hivyo kuwasihi wahitimu hao kuwa wabunifu na kujituma.
Aidha Dkt.Moshi amewapa hadhari wahitihimu hao kuwa kuna matapeli wanaotumia fursa za ajira kutekeleza uovu huo hivyo wanatakiwa kuwa makini na watu kama hao ili wasije wakapoteza kila kitu kwa kuwaamini.
“Kuna watu wanajifanya waajiri wanakupigia simu na kukueleza juu ya maombi yako ya kazi ukisikia suala la kutoa hela ujue huo ni utapeli”. Amesema Dkt.Moshi.
Nae Mshauri wa Wanafunzi Ustawi wa Wanafunzi NIT, Bw.Meshack Kimaro amewataka wahitimu hao wakaitumie elimu yao kwenye ujenzi wa Taifa kwa kuhakikisha wanayasimamia vema malengo yao.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu hao wamesema kuwa watahakikishawanatumia vyema mafunzo waliyoyapata katika ujenzi wa taifa letu kwa ujumla