Tafrija hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma, ilihudhuriwa na watu mbalimbali akiwemoKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa shughuli hiyo.
Waliowakilisha wenzao na kupongezwa kwa Utumishi bora ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji usiku huo ni pamoja na Naibu Kamishna Mstaafu Fikiri Salla, Kamishna Msaidizi Mstaafu Baraza Mvano, Kamishna Msaidizi Mstaafu Bakari Mrisho, Ndg. Rajabu Mfyome, Ndg. Felis Mshana na Bi. Evelyne Kadiva.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, aliwataka wastaafu kutumia kwa uangalifu viinua mgongo vyao watakavyovipata kwani ni kipindi ambacho kila mtu hutolea macho kwa nia ya kuhitaji msaada.
Naye Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, John Masunga aliwashukuru wote waliomaliza muda wao wa Kiutumishi ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na kuwatakia heri katika maisha yao ya ustaafu.
Tafrija hiyo ilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje Mheshimiwa Vita Kawawa (Mb) Makamishna, Viongozi Waaandamizi, Maafisa, Askari na Watumishi wa kada ya kiraia wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.