MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akitoa tamko la Halmashauri Kuu ya Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma (CCM) la Kumpongeza Rais Samia kwa Kazi Nzuri anazoendelea Kuzifanya kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili mbaga,akizungumza wakati wa tamko la Halmashauri Kuu ya Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma (CCM) la Kumpongeza Rais Samia kwa Kazi Nzuri anazoendelea Kuzifanya.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akifanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa fremu 175 za kupangisha zinazojengwa na CCM Mkoa wa Dodoma mara baada ya kutoa tamko la Halmashauri Kuu ya Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma (CCM) la Kumpongeza Rais Samia kwa Kazi Nzuri anazoendelea Kuzifanya.
MUONEKANO wa Mradi wa ujenzi wa fremu 175 za kupangisha zinazojengwa na CCM Mkoa wa Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa,akitoa maelezo mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa fremu 175 za kupangisha zinazojengwa na CCM Mkoa wa Dodoma .
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga ,akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa Frem 174 zinazojengwa na CCM Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kupangisha ambapo mradi ho utakuwa na manufaa makubwa katika kuimaraisha uchumi wa CCM Mkoa.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Meja Mstaafu Johnick Risasi,akipongeza hatua ya ujenzi wa Frem hizo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Mkoa wa Dodoma Neema Majule,akizungumzia lengo la kuanzisha miradi hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia katika kuhakikisha Chama kinajitegemea kiuchumi na kuepuka kuwa omba omba.
………………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
HALMASHAURI Kuu ya Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma (CCM) imetoa tamkoa la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ya kuiongoza serikali pamoja na kuwajali wananchi wake.
Akisoma tamko hilo jijini Dodoma Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwini Mkanwa,amesema kuwa wanampongeza kwa mageuzi makubwa katika sekta ya uchumi,Siasa,Sheria na Diplomasia ambazo zimechagiza kwa kiasi kuweka msukumo wa maendeleo ya wananchi na Miundombinu.
Pia Mkanwa amesema kuwa wanaishukuru serikali Kwa kutenga fedha za kutosha katika bajeti ya 2022/2023 Kwa ajili ya barabara za mzunguko, uwanja wa ndege wa msalato na ukamilishaji wa ikulu chamwino.
“Katika bajeti kuu ya serikali ya iliyosomwa Juni 6 mwaka huu yenye jumla ya sh.trilion 41.5 Mkoa wa Dodoma umetengewa kiasi cha sh.bilion 372 Kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ambapo kiasi kikichotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni sh.bilion 126.8 na sh.bilion 245 imetengwa Kwa ajili ya matumizi ya kawaida,”amesema
Hata hivyo amesema CCM Mkoa wa Dodoma itaendelea kusimamia matumizi mazuri ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa mkoa ikiwemo utolewaji wa mikopo,kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani,kusimamia ujenzi wa zahanati 40,vituo vya afya 21 na hospital za Wilaya sita.
Mkanwa amesema bajeti iliyosomwa na waziri wa fedha bungeni imejielekeza kumkomboa mwananchi wa kawaida kiuchumi,kisasa na kijamii katika sekta ya elimu, afya na Kilimo.
Alibainisha kuwa bajeti hiyo imeeleza kuwa kuanzia mwaka wa fedha ujao mtoto wa kitanzania ataweza elimu bila malipo kuanzia shule ya msingi Hadi kidato sita, pia kupitia wizara ya Kilimo mkulima wa kawaida atapata ahueni ya bei ya chini ya pembejeo bora msaada wa kitaalam.
“Sisi tunasema Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania Samia ameupiga mwingi Kwa jitihada zake za kuitangaza vivutio vya utalii kupitia Filamu ya Royal Tour ambayo imefungulia ongezeko la watalii nchini
Kwa Upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema katika kuhakikisha wanajitegemea kiuchumi wamejenga fremu za kupangisha 174 ambapo watarajia kuvuna zaidi ya sh.bilion 1 Kwa mwaka.
Pia amesema kuwa ujenzi wa mradi huo upo katika hatua ya kukamilika na unatarajia kumalizika ifikapo mwesho wa mwezi huu na umegharimu zaidi ya sh.milion 890.
“Fremu zote zimepata wateja na Kodi ya mwezi ni sh.500,000 na kukamilika Kwa maradi huu kutawezesha kulipa mishahara ya watumishi na posho tunataka Mkoa wetu uwe wa mfano na wajumbe wengine waje kujifunza kwetu na Hadi sasa sisi ndio tunaongoza
Aidha amewataka viongozi wa CCM ngazi ya Wilaya kuhakikisha wanajielekeza katika miradi ya kimkakati ili waweze kujitegemea kiuchumi.