Na John Mapepele.
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa
Tanzania na India zinakwenda kupitia na kuboresha mikataba ya
mashirikiano ya awali kwenye eneo la Utamaduni na Sanaa iliyojiwekea
mwaka 1984 ili kuiboresha iweze kuleta mapinduzi makubwa na ya haraka
kwa faida ya pande zote.

Mhe,
Mchengerwa ameyasema haya leo Juni 17, 2022 akiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dk. Hassan Abbasi wakati alipotembelewa ofisini kwake na
Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan na kufanya
mazungumzo ya kuendeleza mashirikiano kwenye sekta hizo.

Aidha,
amesema mambo mengi yalikubalika baina ya nchi zote mbili hususan
kuendelea kwa tamaduni pia kumekuwa na mambo mengi ambayo yameandikwa
ambayo kuna haja ya kufanya mapitio.

Ameongeza
kuwa katika maongezi hao wamekubaliana kuwa na kituo maalum cha
kuandaa filamu ambacho kitatumika kwa nchi za Afrika mashariki ambapo
baadhi ya wasanii kutoka India watashiriki moja kwa moja kwenye eneo
hili.

Pia
amesema eneo jingine kubwa ambalo wamejadili ni kuhusu umuhimu wa wa
kufanya mkutano mkubwa kuhusu bahari ya Hindi ambao utajumuisha nchi
hizo mbili.

Amesema tamasha hilo litasaidia kuonyesha historia za nchi zote zilikotoka zilipo na zinakoelekea
Aidha,
amesema bahari ya Hindi imebeba historia kubwa ambayo tayari watafiti
kutokana India na Tanzania wamefanya utafiti hivyo ni muhimu kuutumia
utafiti huo kwa faida ya nchi zote.

Naye
Mtaalam na Mtafiti Arindam Mukherjee ambaye ameambatana na Mhe.
Balozi amefafanua kuwa tafiti zinaonesha kuwa Bahari ya Hindi ilikuws
ikitumika kwa miaka mingi kufanya biashara ambapo yapo baadhi ya maeneo
ambayo yamethibitika yamekuwa yakikaliwa na waswahili na pia kumekuwa
na mfanano wa maneno ya kiswahili.